Makamu wa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya, Yahaya Masumbuko akitoa taarifa kikao cha madiwani..
Diwani Hassan Benzi wa kata ya Dosidosi akiwasilisha taarifa ya kamati..Diwani viti maalumu Rael akiwasilisha taarifa..
Na, MOHAMED
HAMAD
MADIWANI wa
halmashauri ya wilayani Kiteto mkoani manyara, wameitaka Serikali kuboresha huduma
ya elimu kwa kuongeza samani na thamani shule, ili wanafunzi waweze kupata haki
ya kupata elimu kwa kiwango stahili
Wakizungumza
kwenye kikao cha baraza la madiwani, baadhi ya madiwani hao walisema, maeneo mengi wanafunzi wanalazimika kusomea chini ya miti na kukaa
chini kwa kukosa vyumba vya madarasa na madawati
Elia Dengea
(CCM), Diwani wa Kata ya Dongo alisema, mazingira ya wanafunzi kupata na
kutolea elimu ni duni katika kata yake, akisema kwa sasa hakuna sababu ya kumlaumu
mwalimu na hata mwanafunzi kwa kufeli kutokana na changamoto hizo
“Huwezi
kutegemea mwalimu kufanya vizuri shuleni wakati anakutana na watoto wanaokaa
chini, tena wengine chini ya miti kutokana na kukosa madawati na hata vitabu, kwa
hili Serikali inatakiwa kuwa macho katika kulishughulikia mapema kabla ya
kujitokeza madhara”
Diwani wa
kata ya Dosidosi, Hassan Benzi (CCM), Kassimu Msonde (CCM) wa Kibaya na Kidawa
Othman Chadema wa Matui, waliitaka Serikali kuhakikisha kuwa inatimiza wajibu
wake wa kutoa huduma hiyo kwa jamii
“Serikali
inatakiwa kuhakikisha ujenzi wa miundombinu ya shule inakuwepo , ili kuepuka
kila kiongozi kujiamulia kufanya atakavyo kwa kutaka kuepuukana na lawama kama miongoni
mwetu wanavyojenga madarasa bila vipimo sahihi, ambayo yanaweza kuleta madhara”
alisema Dengea
Akichangia
hoja hiyo, Emmanuel Mwagala, Afisa elimu msingi alikiri kuwepo kwa baadhi ya
wanafunzi kusomea chini ya miti, na wakiwa wamekaa chini na kuwataka madiwani
kuhamasisha jamii kuchangia elimu kwa lengo la kuiboresha
“Ukaguzi tuliofanya
hivi karibuni, tumebaini kuwepo kwa baadhi ya madarasa, yaliyojengwa chini ya
kiwango tena syiyo na vipimo sahihi, naomba waheshimiwa madiwani kabla ya
kufanya hivyo katika maeneo yenu shirikisheni wataalamu”alisema Mwagala
Mwaka jana
tuliandikisha watoto 36 elfu, mwaka huu tumeongeza uandikishaji na kufikia 46
elfu, watoto wengi nakiri kusoma chini ya miti na hata kukaa chini, ila sasa
madiwani himizeni wananchi kuchangia elimu kwa kukamilisha madarasa alisema
Mwagala
Kwa upande
wake Mkurugenzi mtendaji wa Halamshari ya Wilaya, Tamimu Kambona,
aliwahakikishia madiwani hao kuwa wakijenga vyumba vya madarasa hadi kufikia lenta
kwa kushirikisha wataalamu, serikali itamalizia kama njia ya kushirikishana
katika maendeleo
Mwaisho

Maoni
Chapisha Maoni