Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel, akisoma dua kikao cha baraza la madiwani Kiteto..
Diwani wa kata ya Bwawani, Salmu Ng'ungu, akiwasilisha taarifa ya kata yake..
Eliya Dengea, Diwani kata ya Dongo, akiwasilisha taarifa kikao cha madiwani..
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel kushoto na Mkurugenzi Tamimu Kambona, wakifuatilia mjadala wa kikao cha madiwani..
Wakuu wa Idara wakifuatilia kikao cha madiwani Kiteto..
Katibu wa kikao cha Baraza la madiwani CC. Kituru Othmani akifuatilia kikao
Diwani wa kata ya Dosidosi, Benzi Hassan akiwasilisha taarifa ya kamati ya kamati ya elimu afya na maji..
Paulo Tunyoni diwani wa kata ya Partimbo akiwasilisha taarifa ya mazingira..
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya, Yahaya masumbuko, akiwasilisha taarifa
Madiwani wakifuatilia kikao..
NA. MOHAMED HAMAD
MADIWANI wa
halmashauri ya wilayani Kiteto mkoani manyara, wameitaka Serikali kuongeza kasi
ya kuboresha huduma ya elimu kwa kuongeza samani na thamani shule, ili
wanafunzi waweze kupata haki ya elimu kwa kiwango stahili
Wakizungumza
kwenye baraza la madiwani, wakati wakitoa taarifa za kata madiwani hao
walisema, maeneo mengi wanafunzi wanalazimika
kusomea chini ya miti na kukaa chini kwa kukosa vyumba vya madarasa na madawati
Elia Dengea
(CCM), Diwani wa Kata ya Dongo akitoa taarifa yake alisema, mazingira ya kupata
na kutolea elimu yakiwa duni, hakuna sababu ya kulaumu mwalimu na hata
mwanafunzi kwani hakuna miongoni mwao aliyekamilishiwa miundombinu ya elimu
“Huwezi
kutegemea mwalimu kufanya vizuri shuleni wakati anakutana na watoto waliokaa
chini, tena wengine chini ya miti kutokana na kukosa madawati na hata vitabu, kwa
hili Serikali inatakiwa kuwa macho katika kulishughulikia”
Maoni
Chapisha Maoni