Waandishi Manyara wapigwa msasa..

Mkuu wa Wilaya ya Babati, DC Raymond Mushi, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr. Joel Nkaya Bendera Siku ya uhuru wa vyombo vya habari..
 Waandishi wa habari wa mkoa wa Manyara wakifuatilia jambo siku ya uhuru wa vyombo vya habari..



Mkurugenzi mtendaji wa halm ya wilaya ya Mbulu, Hadson Kamoga, akikitoa somo na salamu kwa wanahabari wa mkoa wa Manyara..
 Hadson Kamoga DED Mbulu..
 Meneja wa mfuko wa bima ya Taifa NHIF mkoa wa manyara, Hance Mwankenjwa, akiwasilisha mada ya umuhimu wa kujiunga na mfuko.. 
 Meneja wa BAWASA Manyara akiwasilisha mada ya maji..
 Kiongozi wa Jeshi la Polisi, ambaye pia ni mdau wa habari akitoa salamu kwa wanahabari wa Manyara..





Na,MOHAMED HAMAD

CHAMA cha waandishi wa habari, mkoani Manyara MAMEC, kimeungana na waandishi wengine kuadhimisha uhuru wa vyombo vya habari, ambapo pamoja na mambo mengine wametaja changamoto na mafanikio katika tasnia ya habari..

Miongoni mwa changamoto zilizotajwa ni pamoja na kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na maslahi madogo kwa wanahabari, huku wakitakiwa kuendelea kuwa na subra katika kazi hizo na kufanya kazi kwa weledi..

Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa sheria ya huduma ya vyombo vya habari, Hadson Kamoga, Mkurugenzi mtendaji wa Halamshauri ya Mbulu, alimpongeza Rais Dr. John pombe Magufuli kwa kusaini sheria ya huduma kwa vyombo vya habari akisema, itakuwa na tija katika tasnia ya habari hasa katika kipindi hiki chenye changamoto akisema sheria ya makosa ya mitandaoni ni hatari watu wawe macho

Mkurugenzi Kamoga amewataka wanahabari kuwa na utamaduni wa kusoma sheria mbalimbali zinazowahusu na zingine ili ziwasaidie katika kazi zao wasiweze kufanya kazi kwa mazoea na kuwataka kutoka katika kuripoti wajielekeze kuandika habari za uchunguzi

Kwa upande wake meneja wa mfuko wa bima ya afya Taifa NHIF mkoa wa manyara, Hance Mwankenjwa, akiwasilisha mada ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo alisema, vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuelimisha umma juu ya mambo mbalimbali yanayowahusu

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Manyara, Charles Masayanyika,  kwa niaba ya chama alimshukuru mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati kwa kuwapa kiwanja, pamoja wadau wengine  Chama kupatiwa eneo la ujenzi wa ofisi, pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kuchangia saruji na mchanga kwaajili ya kuanza ujenzi huo


Maoni