UCRT wawezesha wananchi 44 kupata hati za Kimila Kiteto

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto DC Tumaini Magessa, katika mkutano na wananchi wa vijiji vya Ngabolo na Ndedo kugawa hati za kimila chini ya shirika lisilo la kiserikali la  Ujamaa Community Resource Team (UCRT) lenye makao makuu Arusha..
Wakili Edward Lekaita akifafanua jambo..
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngabolo akifafanua jambo baada ya kugawanywa hati za kimila..
Picha ya pamoja DC Tumaini Magessa, Mkurugenzi mtendaji wa halm ya wilaya ya Kiteto Tamimu Kambona na uongozi wa UCRT, Akiwemo wakili Edward Lekaita..
 Viongozi wa kimila wa jamii ya kifugaji maasai ( Laigwanani)..wakifuatilia jambo..
  Viongozi wa kimila wa jamii ya kifugaji maasai ( Laigwanani)..wakifuatilia jambo..
Wananchi wa Kijiji cha Ngabolo wakifuatilia mkutano..
Wananchi wa Kijiji cha Ngabolo wakifuatilia mkutano..
 Wananchi wa Kijiji cha Ngabolo wakifuatilia mkutano..
 Wananchi wa Kijiji cha Ngabolo wakifuatilia mkutano..


 Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Ndedo, akikabidhiwa hati ya kimila na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa..
Mkuu wa wilaya DC Tumaini Magessa kushoto na Mkurugenzi Tamimu kambona baada ya kuvalishwa vazo la kimasai..


NA. MOHAMED HAMAD
WILAYA ya Kiteto ni moja kati ya wilaya Mkoani manyara zenye changamoto ya migogoro ya ardhi, iliyosababisha watu kupoteza maisha kwa kugombania ardhi..

Hali hiyo imesukuma wadau wa maendeleo, likiwemo shirika la UCRT lenye makao yake makuu Arusha, kuja kutoa mafunzo ya namna ya kumilika hati za kimila na kusaidiwa kupata hati za kimila kwa wanawake wa jamii ya Kifugaji 43 na mwanaume mmoja 

Lengo ni kuondoa mfume Dume unaodaiwa kushamiri katika kabila hilo ambao linadumisha mila tofauti na makabila mengine wilayani hapa..

Baadhi ya wanufaika wa hati hizo walishukuru kupatiwa na kuomba Serikali kuona namna ya kuendelea kuwapiga jeki ili kujikwamua na umaskini wa kipato

Kwa upande wake Edward Lekaita, ( Wakili aliwashukuru jamii hiyo kwa kujitolea muda wao kufuatilia namna ya kumiliki ardhi..

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Mgessa, pamoja na kuwapa pongezi hizo, aliwataka wajumbe hao kuwa chachu kwa wenzao ili waweze kuongezena wenye mahitaji hayo

Mwisho







Maoni