Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngapapa Ngalama Oloiboo akiendesha mkutano wa wananchi kama ishara ya namna walivyoweza kukubaliana kuunda eneo la pamoja (OLENGAPA) kwaajili ya malisho
Mainge Lemalali Diwani wa kata ya Lengatei, mbele ya timu ya wajumbe 30 akifafanua jambo kuhusu namna walivyoweza kuunda eneo la pamoja la vijiji vitatu kwaajili ya malisho ya mifugo yao (OLENGAPA)
Mmoja wa wanajamii ya kifugaji maasai Seenoi Alakara akifafanua jambo namna walivyuweza kushiriki katika kuunda eneo la pamoja la malisho la (OLENGAPA)
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Orkitikiti wakifuatilia taarifa za mafunzo zinazotolewa kwa wajumbe 30 kutoka nchi mbalimbali waliofika kijijini kwao
Wananchi wa Kijiji cha Orikitikiti wakifuatilia jambo katika kikao
Wananchi wa Kijiji cha Orikitikiti wakifuatilia jambo katika kikao
Wajumbe kutoka nchi za Italy, Nigeria, na Kenya wakifuatilia jambo ziara ya mafunzo Kiteto Manyara Tanzania
Diwani wa kata ya Lengatei, Mainge Lemalali akimkabidhi taarifa mmoja wa viongozi wa timu iliyokuja kujifunzo katika Kijiji chake cha Orkitikiti kata ya Lengatei Kiteto Manyara Tanzania
Wajumbe kutoka nje ya Nchi wakuwa na wenyeji wao maasai chini ya diwani Mainge Lemalali
Mmoja wa maafisa kutoka Wizara ya mifugo Bw.Victor Mwita akifafanua jambo kwa jamii ya kifugaji maasai wa Kijiji cha Orkitikiti kata ya Lengatei waliotembelewa na wajumbe 30 kutoka nje ya nchi
Wajumbe kutoka nje ya nchi wakiwa Kijiji Orkitikiti wakifuatilia jambo
Wajumbe kutoka nje ya nchi wakiwa Kijiji Orkitikiti wakifuatilia jambo
Victer Mwita kutoka Wizara ya mifugo akimkabidhi cheti mwenyekiti wa Bodi ya shirika la KINNAPA Alais Nangoro kama ishara ya jitihada za kuwezesha mafanikio hayo ya zoezi hilo
Diwani wa kata ya Partimbo Paulo Tunyoni akionyesha Makamishna kutoka Nigeria rungu linalotumiwa na jamii ya kifugaji maasai kwa viongozi wa kimila
Mwenyekiti wa Bodi ya KINNAPA Alais Nangoro akiteta jambo na wageni hao
Paulina Ngurumwa akimpamba mmoja wa wageni kutoka Italia ambaye ni kiongozi wa msafara kama moja ya ishara ya ukarimu kwa jamii ya kifugaji
Laura Fantini kiongozi wa msafara hiyo akitetoa jambo na mratibu wa shirika la KINNAPA Abraham Akilimali katika kijiji cha Orkitikiti Kiteto Manyara TANZANIA
Makamishna kutoka Nigeria wakipiga makofi kama ishara ya kufurajishwa na jambo lililotolewa katika ziara hiyo kijiji cha Orkitikiti
Jamii ya Kifugaji wakifuatilia jambo kwenye kikao..
Wajumbe kutoka nchi mbalimbali Afrika na nje wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya siku mbili chini ya Shirika la KINNAPA katika Kijiji cha Orkitikiti kata ya Lengatei Kiteto Manyara Tanzania
Mohamed Hamad Mwandishi wa Hamari kutoka Tanzania kulia akiwa na mpiga picha kwenye ziara ya jopo la watu 30 waliofika ziara ya mafunzo Kiteto Manyara Tanzania
Na, MOHAMED HAMAD
JOPO la watu 30 kutoka nchi za Naigeria, Italiya na Kenya limefanya ziara ya kimafunzo katika Kijiji cha Orkitikiti kata ya Lengatei Wilayani Kiteto mkoani Manyara Tanzania, kwaajili ya kujifunzo na kuona eneo lililotengwa la nyanda za malisho ya pamoja la OLENGAPA
Jumla ya vijiji vitatu katika kata za Lengatei na Kijungu ambavyo ni Orkitikiti, Lerug na Ngapapa kwa pamoja walitenga eneo la hekta 20,706.73 kwaajili ya malisho ya pamoja kwa lengo la kupunguza migogoro ardhi kati ya wakulima na wafugaji
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi shirika la KINNAPA Alayce Nangoro mbele ya wajumbe hao alisema kazi hiyo haikuwa rahisi kwani iliwalazimu kutumia muda mwingi kushirikisha wananchi na wadau mbalimbali kuelewa na kufanya maamuzi hayo
Akisoma risala kwa wageni hao Diwani wa kata ya Lengatei Mainge Lemalali alisema wazo la kuwa na eneo la pamoja lilitokana na bwawa la Orkitikiti lililokuwa limechimbwa kabla ya Uhuru wa nchi ya Tanzania 1957 ambalo lilitumiwa na wananchi wa vijiji hivyo
Alisema bwawa hilo liliwasaidia kwa muda huo kwaajili ya matumizi ya binadamu na mifugo, ambapo ulipofika mwaka 1982 vijiji hivyo vilisajiliwa na kuwa na uongozi wao ambao umeweza kufanikisha wazo la kuunda nyanda za pamoja za malisho
"Hapo awali tulitumia sheria za kimila kuhakikisha mambo yanaenda, aliyekosea ndani ya jamii yetu alitozwa faini ya DUME la ng'ombe hadi tulipoweza kufikia hatua hii, hivyo sio kazi rahisi kama mnavyoweza kufikiri alisema Mainge
Alisema nyanda za malisho ya pamoja OLENGAPA na zimesajiliwa kisheria na tayari zimeanza kutumika ingawa kazi kubwa ni kuanza kupanda nyasi za malisho zaidi kuboresha malengo mahususi ya uanzishwaji wa nyanda hizo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni