Kiteto waunda umoja wa Dini mbalimbali

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kikristo Tanzania Mch Kanon Moses Matonya akizungumza na baadhi ya wanachama wa vikundi vya vicoba mjini Kibaya Kiteto Manyara Tanzania 
Cherrles Machibya mratibu wa vicoba Kiteto akimkaribisha mkurugenzi wa Jumuia ya Kikristo Tanzania CCT ili aweze kuzungumza na wanachama wa vicoba mjini Kibaya
Wanachama wa vicoba Kibaya wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kikristo Tanzania Mch Kanon Moses Matonya 
Wanachama wa vicoba Kibaya wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kikristo Tanzania Mch Kanon Moses Matonya 
Viongozi wa dini mbalimbali Kiteto wakimlaki Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kikristo Tanzania Mch Kanon Moses Matonya
Emmanuel Joseph katika kikao na viongozi wa dini mbalimbali Kiteto wakijadili namna ya kushirikiana katika kuwahudumia waumini wao
Salamu baada ya kukutana kwa mara ya kwanza kwa viongozi wa dini mbalimbali Kiteto
Viongozi wa Jumuia ya Kikristo Tanzania katika mkutano na wanachama wa vikoba kata ya Ilkiushbour Kiteto Manyara
Kikao cha viongozi wa CCT Tanzania na wanachama wa vicoba Ilkiushbour Kiteto

NA MOHAMED HAMAD
JUMUIA YA KIKRISTO Tanzania na viongozi wa BAKWATA Kiteto wameungana kwa pamoja kama watoa huduma ya IMANI kwa watu wao kujadili namna bora ya kutoa huduma hiyo bila kuhitilafiana

Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamezungumzia namna ya kuwaimarisha waumini kiimani, Kiuchuni ili waweze kuwa wema wenye matumaini ya malipo  siku ya mwisho

Wakiwa katika kikao cha pamoja katika Jengo la maendeleo ya jamii Community Center Kibaya, viongozi hao wamesema ili muumuni aweze kumcha Mungu anatakiwa kuimarika kiuchumi

Sambamba na hilo wamekubaliana kwa pamoja kila muumini ana wajibu wa kuheshimu imani ya mwenzake anapokuwa katika ibada tofauti na ilivyokuwa awali kuwa walionana maadui

Akizungumza kwa hisia kali mmoja wa wajume hao Mama Ndolosi alisema awali haikuwa rahisi kiongozi wa dini ya Kiislamu kushirikiana na wakristo katika mambo ya kijamii tofauti na ilivyo sasa

Akizungumza mbele ya viongozi hao Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kikristo Tanzania Mch Kanon Moses Matonya alisema DINI ni milango ya kumfanya mtu aweze kumfahamu Mungu na kumfuata

" Hatuna sababu ya kuonana maadui katika Dunia hii.. kwani ajuaye ni Mungu pekee na wala sio mwanadamu.. ni vyema kuheshimiana katika imani zetu"

Naye Maalim Jumaa Mohamed Hicha katika kikao hicho alisema kuheshimiana kwa waumini wa dini mbalimbali kunajenga ustaarabu katika imani na kuwataka kila kiongozi kuona haja ya kulinda mahusiano hayo

Abassy Famau ni katibu wa umaja wa dini mbalimbali akichangia hayo alisema jitihada za kuimarisha umoja huo zinaendelea ambapo sasa wamefikia hatua ya kutengeneza makubaliano ya pamoja kwa viongozi wa dini mbalimbali Kiteto

Mwisho




Maoni