Mkesha wa Mwenge waibua 2 wenye VVU Ukimwi Kiteto

Mwenge wa Uhuru Kiteto 2017
Eneo la mkesha wa mwenge wa Uhuru mwaka 2017 mjini Kibaya Kiteto Manyara
Kitengo cha upimaji wa VVU Ukimwi eneo la mkesha wa mwenge mjini Kibaya Kiteto Manyara
Kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akipanda mti shule ya Sekondari Engusero kama ishara ya kuzuia jangwa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Bi. Salome akipanda mti shele ya Sekondari Engusero Kiteto



Mkesha wa Mwenge waibua 2 wenye VVU Ukimwi Kiteto

Na, MOHAMED HAMAD
ZOEZI la upimaji wa hiyari maambukizi ya VVU Ukimwi kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru mjini Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara, limebaini watu wawili kuishi na maambukizi kati ya 369 waliopima

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, DC Tumaini Magessa akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour alisema zoezi hilo limefanyika kwa hiyari sambamba na uchangiaji wa damu salama ambapo lita 23 zilipatikana

Alitaja lengo la upimaji huo kuwa ni kuwafanya watu waweze kuishi kwa kujua afya zao ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua aina ya kazi kulingana na afya zao sambamba na kuanzishiwa dawa kwa wakati

Awali akizungumza na wananchi wa miji midogo ya Kibaya na Matui, kiongozi huyo wa mbio za mwenge Kitaifa aliwataka wananchi wa Kiteto kuendelea kuchukua tahadhari juu ya gonjwa hatari la ukimwi ambalo ni adui wa Taifa

“ Ndugu zangu wananchi wa mji wa matui, gonjwa hili la Ukimwi ni tishio kwa Taifa letu.. tunapaswa kuchukua tahadhari sambamba na dawa za kulevya kwani kwa pamoja nguvu kazi ya Taifa vijana wetu wanapungua kwa vifo kila kukicha”

Alisema ujumbe wa Mwenge mwaka huu unawataka wananchi kushiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi akidai, Taifa litafanikiwa kupata maendeleo endapo watu wake watakuwa na afya njema

Kwa upande wa baadhi ya wananchi waliozungumza na MTANZANIA kuhusiana na ujumbe huo walisema, Serikali inatakiwa kusimamia sheria kikamilifu kukabiliana na baadhi ya watu wanaoambukiza Ukimwi kwa maksudi

Walisema pamoja na kuwepo kwa sheria zinazokataza watu kuambukizana kwa maksudi baadhi yao wamekuwa wakiambukiza huku kukiwa na ukimya uliokidhiri hasa katika maeneo ya vijijini juu ya gonjwa hilo

Miradi nane ya thamani ya tsh mil 750, 571,120 imepitiwa na mwenge wa Uhuru  mmoja umefunguliwa, mmoja umewekewa jiwe la msingi, miradi mine imezinduliwa na miwili imekaguliwa

 Miradi hiyo ni ujenzi wa ward ya wanawakena watoto kituo cha afya cha Matui wa zaidi ya mil 37, Kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti na kusaga unga wa mahindi cha Kwadelo cha zaidi ya mil 400 kata ya Matui, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vya zaidi ya mil 26 kata ya Engusero,na mradi wa maji kaloleni wa zaidi ya mil 255


Mwisho

Maoni