Mwenge wa Uhuru Kiteto 2017
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kiwilaya..
Mkuu wa wilaya ya Kiteto DC Tumaini Magesa akisubiri kupokea Mwenge Kijiji cha Kiperesa..
Ndaki Stefano akionyesha furaha baada ya kupogea ugeni wa Mwenge Kiteto
Mkuu wa wilaya ya Kiteto DC Tumaini Magessa akipokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Babati Manyara
Mwenge wa Uhuri baada ya Kuwasili Kijiji cha Kiperesa Kiteto Manyara
Uvikaji wa skafu kwa wakimbiza mwenge Kitaifa
Kamati ya Ulinzi na usalama Kiteto
Afisa mtendaji kata ya Matui akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi ward Zahanati ya Matui Kiteto Manyara..
Kiongozi wa mbio za Mwenge Amour Hamad Amour akikagua mradi wa Ujenzi wa ward ya zahanati Matui Kiteto Manyara
Kiongozi wa mbio za Mwenge akionyesha mfano wa kuunga mkono jitihada za ujenzi ward ya Matui Kiteto Manyara
Kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa akisaidia jitihada za ujenzi zahanati ward ya kata ya Matui
Mkuu wa Polisi Kiteto Patrick Kimaro maarufu Sabasita alihakikisha ulinzi unaimarika
Kiongozi wa Mbio za Mwenge akikagua kiwanda cha mtu binafsi cha kukamua alizeti kinachomilikiwa na Hamadi Kwadelo kata ya Matui Kiteto Manyara
Kiongozi wa Mbio za Mwenge akizungumza na wananchi wa Kata ya Matui
Mwenge wa Uhuru ukiwasili shule ya Sec Engusero kufungua mradi wa madarasa mawili ya kidato cha tano na sita
Uzinduzi wa madarasa mawili ya kidato cha tano na sita sec ya Engusero Kiteto
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru akipanda mti Shule ya Sekondari Engusero Kiteto
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa akipanda mti Sec ya Engusero Kiteto Manyara
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Salome akipanda mtu wa kumbukumbu Sec ya Engusero
Kamati ya Ulinzi na usalama Kiteto katiuka picha ya Pamoja baada ya kupokea Mwenge
Eneo la mkesha wa mwenge halaiki wakiimba nyimbo mbalimbali za Tanzania
Baada ya kumalizika Risala ya Utii eneo la mkesha uwanja wa mpira wa miguu mjini Kibaya
Wakimbiza MWENGE wakitokea Kiteto kutaka kukabidhi Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Simanjiro
Mwenge wa Uhuru Simajiro
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa akipongezwa baada ya kukabidhi Mwenge
Furaha baada ya Kiteto kukabidhi Mwenge Wilaya ya Simanjiro
Mkurugenzi wa Kiteto Tamimu Kambona akiteta jambo na Mkurugenzi wa halm ya Simanjiro Bw Myenzi
NA MOHAMED HAMAD
MWENGE wa Uhuru umewasili Kiteto mwaka huu wa 2017 ukitokea Babati na kupokelewa Kijiji cha Kiperesa na baadaye kuelekea kata ya matui ambako ulikagua mradi wa Ujenzi wa ward zahanati ya Matui
katika kata hiyo Mwenye ulizindua kiwanda cha kukamua alizeti na kusaga sembe cha Bw Hamad Kwadelo kisha kiongozi wa Mbio za Mwenge Amour Hamad Amour kuongea na wananchi wa mji mdogo wa Matui
Katika mbio hizo za Mwenge ulielekea Kata ya Engusero na kuzindua madarasa mawili ya Kidato cha tano na sita na kuzindua zoezi la upandaji wa miti ambapo lilitakiwa kila mtu aweze kupanda miti minne kama nji mojawapo ya kukabiliana na ukame
Mwenge wa Uhuru ulielekea Kibaya ambapo ulizindua mradi wa maji chini ya wahisani kutoka Misri ambao utasaidia wananchi wa kata ya Kaloleni na Kibata na kisha kuelekeza uwanja wa mpira wa miguu ambapo kiongozi wa mbio hizo alikagua miradi mbalimbali katika mabanda maalumu yaliyokuwa yameandaliwa
Baada ya ukaguzi huo na kusomwa Risala ya Utii kwa Mhe Rais na Katibu Tawala wa Wilaya Ndaki Stephano, mkesha ukafanyika katika viunga hivyo vya uwanja wa mpira wa miguu mjini Kibaya
Asubuhi Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa kwenda kukabidhiwa Wilaya ya Simanjiri ambapo makabidhiano hayo yalifanyika katika Kijiji cha Londroges iliyopo wilaya ya Simajiro..
Maoni
Chapisha Maoni