Shule ya msingi Boma Sidani Kiteto yapata tuzo

Epafra Lema mwalimu mkuu wa shule ya msingi Boma Sidan akionyesha Wazazi baadhi ya zawadi walizopewa kiwilaya Kimkoa na hata Taifa kutokana na kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya darasa la saba
Epafra Lema mwalimu Mkuu shule ya msingi Boma akionyesha Kombe wazazi kutokana na ushindi huo
Zawadi kwa za shule kwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa
Mwalimu Lema "Hizi ni zawadi tulizopewa"


NA MOHAMED HAMAD
SHULE ya msingi Boma Sidan, iliyopo wilayani Kiteto mkoani Manyara, imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba hali inayofanya waweze kupongezwa kwa jitihada zao

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutokana na mafanikio hayo imeelezwa siri ya mafanikio, wazazi wamekuwa na utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao kwa kushirikiana na waalimu

Abubakar Mrisho Makamu mwenyekiti wa shule hiyo akizungumza na wazazi katika moja ya kikao cha maendeleo ya shule hiyo alisema, anasikitishwa na nafasi ya pili waliyopata Kimkoa kutokana na mazoea waliyoYapata ya kuwa wakwanza kila mwaka

Hali hiyo imewasukuma wazazi kukutana katika kikao cha dharura na kuazimia kuunga mkono Jitihada za Walimu kufundisha hadi waweze kurejea nafasi yao ya kwanza Kimkoa 

"Wazazi tumechukizwa sana na matokeo ya awamu hii..ila sasa tumejipanga kuhakikisha kuwa tunarejea upya katika nafasi yetu ya kwanza kimkoa kwani tunajua jitihada za walimu katika shule yetu"

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa shule hiyo Bw. MNUO alisema wameweka mipango na mikakati katika kuifanya shule kuongoza kila mwaka Kimkoa na hata Kitaifa

Mwisho

Maoni