Mkuu wa wilaya ya Kiteto, TUMAINI MAGESSA akisisitiza wananchi kuachana na vitendo vya rushwa
3 Jela kwa kuomba na kupokea rushwa
Kiteto
Na, MWANDISHI WETU
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilayani
Kiteto mkoani Manyara, imewatia hatiani watu watatu wa kada mbalimbali kwa
makosa ya kuomba na kupokea rushwa
Waliotiwa hatiani ni aliyekuwa diwani
wa kata ya Ndirigishi Chitu Baini (CCM), Katibu wa msitu wa jamii SULEDO,
Bakari Hemed na Katibu wa baraza la kata ya Matui Nicodemus Bayo
Akitoa hukumu kwa Diwani Chitu Baini
(CCM) aliyeomba na kupokea rushwa ya laki tano, hakimu Elimo Masawe alisema mahakama
imejiridhisha kwenda jela miaka mitatu ama faini ya mil moja kwa makosa mawili
kuomba na kupokea rushwa
Katika tukio lingine katibu wa msitu
wa jamii SULEDO, ulioundwa na kata tatu za Lengatei, Sunya na Dongo, Bakari
Hemed amehukumiwa kwenda jela mika mitatu bila faini kwa makosa mawili ya kuomba
na kupokea rushwa ya tsh laki saba na nusu
Akisoma shitaka hiyo Hakimu Masawe
alisema awali katibu huyo aliwakamata watu watatu watatu kwa madai ya kuvamia
eneo la hifadhi ya msitu wa jamii SULEDO na kuwaweka ndani kwa siku tatu
mfululizo
Katika mahakama hiyo katibu wa baraza
la ardhi kata ya Matui Necodemus Bayo, alitiwa hatiani kwa kuomba na kupokea rushwa
ya elfu 40,000 ili aweze kutoa upendeleo kwa mmoja wa wananchi katika baraza
hilo
Kwa mujibu wa Mwendesha mashitaka wa
kikosi cha kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Isdory Kiyando mahakamani
hapo kwa nyakati tofauti alimwomba hakimu kutoa kutoa adhabu kali kwa
watuhumiwa hao
Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao
kumetokana na mafanikio ya huduma ya longa nasi ya kupiga simu ya bure (113)
ambayo ilifanikisha kukamatwa watuhumiwa hao wakiomba na kupokea rushwa
mwisho
Maoni
Chapisha Maoni