Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa..
DC Kiteto awaasa wananchi kuchimba
vyoo
Na, MOHAMED
HAMAD
MKUU wa
wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa, amewataka wananchi
wilayani humo kuchimba vyoo kwenye makazi yao kuepuka magonjwa ya milipuko
Akizungumza
na wananchi wa mji wa Kibaya, mhandisi Magessa alisema, taarifa alizonazo idadi
kubwa ya makazi ya wananchi wilayani humo
hayana matundu ya vyoo
Hawezi
kuishi ukiwa na afya njema kama makazi yeko hayazingatii usafi, kuwa na vyoo ni
kiashiria mojawapo cha kuonyesha mnazingatia afya zenu
Alisema
msako mkali utaanza kwa wamiliki wa kaya ambazo hawana matundu ya vyoo katika
makazi yao ili kuwashurutisha waweze kuwa nayo kuepuka magonjwa ya mlipuko
Akizungumza
na MTANZANIA diwani wa kata ya Lengatei Mainge Lemalali alisema wafugaji wa
jamii ya kimaasai Kiteto hawana utamaduni wa kuwa na matundu ya vyoo
Alisema
katika maisha yao hujisaidia porini jambo ambalo kitaalamu linaweza kusababisha
madhara kama vile homa za matumbo na hata kipindupindu
Kwa upande
wa baadhi ya wananchi wakizungumzia agizo hilo walisema, lengo la Serikali ni
jema isipokuwa tatizo ni elimu sahihi na kwa wakati ili waweze kufanya maamuzi sahihi
Kemaa
Kisiyoo mmoja wa wanajamii ya kifugaji (maasai) Kiteto alisema, wamekuwa na
utamaduni siku zote wa kuhamahama na mifugo hivyo sio rahisi kuwa na choo cha
kudumu
MWISHO.
Maoni
Chapisha Maoni