Shamba la mipapai lililopo Same mkoani Kilimanjaro, àmbalo Mkurugenzi wa kampuni ya Namaingo Biubwa Ibrahimu amefika kuona jitihada za vikundi vya wajasiriamali
Jitihada za vikundi vya wajasiriamali Same zaonekana kwà kuanza uzalishaji kwa wanavikundi chini ya Kampuni ya Namaingo
Na MOHAMED HAMAD
VIKUÑDI vya wajasiriamali KANDA ya kaskazini Arusha na Kilimanjaro vimeanza kunufaika na kampuni ya Namaingo kwa kuanzisha Miradi ya kuwainua kiuchumi
Biubwa Ibrahimu, ni Mkurugenzi wa kampuni ya Namaingo, yenye makao yake makuu Dar..akiongea na mwanganamatukio alisema lengo la kampuni yake ni kuwajengea wananchi uwezo wakiuchumi
Alisema Namaingo inajukumu la kuwaunganisha wajasiriamali na fursa mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha,wataalamu mbalimbali wa kilimo na mifugo, pamoja na masoko
Katika hahatua hiyo alisema maamuzi ya kuwa maskini au tajiri ni ya mtu mwenyewe baada ya kupatiwa elimu ya ujasiria Mali ambayo hutolewa na kampuni yake
Kwa sasa kampuni ya Namaingo imetandaa nchi nzima ambapo Mkurugenzi huyo anaendelea na ziara kuzunguka nchi nzima kutoa elimu hiyo
Akiwa Manyara Arusha na Kilimanjaro, baadhi ya wanachama walifurahishwa na elimu hiyo wakisema lililobaki ni wajibu wa wao kufanya maamuzi na kumwomba Mkurugenzi huyo kuendeleza jitihada kwa watanzania wengine zaidi ili kwa pamoja waondokane na umaskini wa kipato
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni