Kiteto nyumba ya mwalimu yatumika kama darasa

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa katika mahafali ya darasa la saba shule ya msingi Indorokoni kata ya Njoro mwaka 2017
Mkuu wa wilaya ya Kiteto akisisitiza jambo
Washiriki wa mahafali ya darasa la saba shule ya msingi Indorokon Kiteto..
Wataalam katika mahafali shule ya msingi Indorokoni..
Mwalimu Rasi, Mariamu Bakari na mwenyekiti wa shule kulia wakifuatilia jambo..
Wanafunzi shule ya msingi Indorokoni wakifuatilia matukio mahafali ya kuaga darasa la saba 2017
Wanafunzi shule ya msingi Indorokoni wakifuatilia matukio mahafali ya kuaga darasa la saba 2017
Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi Indorokoni wakifuatilia jambo..
Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi Indorokoni mara baada ya kukabidhiwa vyeti..
Washiriki katika mahafali..
Majengo ya shule ya msingi Indorokoni
Mkuu wa Wilaya mara baada ya kuwasili shule ya msingi Indorokoni katika mahafali ya darasa la saba 2017..




Nyumba ya mwalimu yatumika kama darasa Kiteto..
·       
               .Walimu waingia mitaani kupanga

Na, MOHAMED HAMAD
Nyumba ya mwalimu wa shule ya msingi Indorokoni kata ya Njoro wilayani Kiteto Mkoani Manyara, inatumika kama darasa kwaajili ya wanafunzi kusomea wakiwa ndani

Shule ilifunguliwa mwaka 2011 kwa lengo la kuondoa adha ya wanafunzi jamii ya kifugaji maasai kutembea umbali mrefu na baada ya kufunguliwa changamoto zaidi zimejitokeza

Akizungumza hayo Rehema Cheleleo diwani viti maamlumu (CCM) alisema, hali hiyo imechangiwa na tabia za baadhi ya wafugaji kutoona umuhimu wa elimu

Alisema pamoja na jitihada za Serikali kuboresha elimu bado hawaoni haja kusomesha watoto wao na kuiomba Serikali kuongeza nguvu katika hamasa kwa jamii hiyo

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rashidi Itungi alisema shule ina vyumba vitatu vya madarasa, nyumba moja wa mwalimu inayotumika kama darasa, choo na uhaba wa walimu huku ikiwa na wanafunzi 400

Alisema pamoja na changamoto hizo, mwaka huu jumla ya wanafunzi 15 kati ya 23 waliofanya mtihani wa Taifa wamefaulu kujiunga na Sekondari ambapo ameiomba Serikali kuona haja ya hamasa kwa jamii hiyo

Mwenyekiti wa Kijiji cha Indorokoni Sindilo Itemi, akizungumza mbele ya mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa alisema jamii hiyo iko tayari kuchangia sherehe zaidi kuliko elimu

Ukifuatilia sherehe za Kifugaji (maasai) mtu anachangiwa zaidi ya mil tano hadi kumi, lakini ukimtaka achangie maendeleo ya elimu utakosana naye

“Tumeamua kuunda sheria ndogo..ambazo zitatumika kuwashurutisha watu hawa, zimewasilishwa kwa mkurugenzi mtendaji na baadaye kikao cha baraza la madiwani Kiteto ili zipitishwe”

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara Tumaini Magessa, amekiri kuwepo kwa uchangiaji hafifu wa elimu kwa jamii hiyo akisema wanatabia ya kuwaozesha watoto wa kike ili wapate mali na wakiume kuchunga mifugo


mwisho

Maoni