Kiteto warithi kasi ya Rais Magufuli

Mkuu wa wilaya ya Kiteto TUMAINI MAGESSA 




Kiteto warithi kasi ya Rais Magufuli



Na MOHAMED HAMAD
Kwa hali ya kawaida bila upendeleo kinachoendelea wilayani Kiteto mkoani Manyara ni ambacho Rais John Pombe Magufuli anataka wananchi wafanyiwe

Wilaya ya Kiteto ilikabiliwa na tatizo la baadhi ya viongozi wao kuwawajibika ipasavyo hali iliyofanya wananchi kuishi kwa kuwalalamikia  hadharani

Hali hii ilifanya kila mtumishi wa Serikali anayefika awe na hofu ya kufanya kazi kutokana na msimamo wa wananchi hao ambao awali walikata tamaa dhidi ya viongozi hao

Wakati mwingini kutokana na misimamo hiyo baadhi ya watumishi wa Serikali walionekana kuomba uhamisho kwenda wilaya zingine kuepuka msimamo huo wa wananchi hao

Wakati mwingine wananchi hao walionekana kuwa na hasira  ya kutopata huduma za jamii kwa kiwango stahili hali iliyofanya waone hawawezi tena kupata viongozi  watakaowapatia huduma hizo

Wananchi hao wamepata viongozi ambao kwa utendaji wao wa kazi wameonekana kusahaulisha yaliyopita  na kujiona kuwa nao ni sehemu ya watu ambao wanahaki

Wanaotajwa kuwa nguzo muhimu na kuwapa faraja wananchi hao ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, amedaiwa kuwa mwenye hekima na busara katika maamuzi

Busara za kiongozi huyu zimetajwa kupunguza  hasira na hisia mbalimbali za wananchi kuwa kila jambo litokea lazima lifikishwe kwa viongozi wa ngazi za juu kama Mawaziri na hata Mheshimiwa Rais

Kila mara wananchi walionekana kuvutana na baadhi ya viongozi wao lakini kutokana na busara hizo wamerejea katika hali zao na kuwa wamoja pamoja na viongozi wao

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya naye ametajwa kupunguza machungu ya wananchi hao kwa kusogeza huduma za jamii japo kwa kiasi flani na kuonekana machoni mwao

Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na uezekaji wa madarasa ya shule ambayo ilikuwa ngumu kuezeka kwa madai ya kutokuwa na fedha, uimarishaji wa vituo vya afya, ujenzi wa soko la kibaya, na ujenzi wa miundombinu ya barabara 

Sekta zingine zilizotajwa ni pamoja na maboresho katika Jeshi la Polisi ambapo wamepatikana viongozi wanaofanya kazi kwa uadilifu na kupunguza manununiko kwa wananchi

Hali hii ikiendelea kila mtumishi kutimiza wajibu wake malalamiko haya ya wananchi yatapungua na kupatiwa huduma za jamii kama lilivyo kusudio


Mwisho

Maoni