Wanachama wa chama cha walimu Kiteto CWT katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa wilaya, Mhandisi Tumaini Magessa..
Mwenyekiti wa CWT Kiteto, Paulo Gwacha akimkaribisha mgeni rasmi na mkuu wa wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumaini Magessa, kuhutubia mkutano mkuu wa chama 2017..
Mkuu wa wilaya ya Kiteto mwenye nguo nyeupe katikati picha ya pamoja na uongozi wa CWT na kamati yake ya ulinzi na usalama kikao cha CWT
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya akizungumza jambo kikao cha chama cha walimu Kiteto
Katibu wa CWT Kiteto Waziri Banga kulia akiteta na mwenyekiti wake Paulo Gwacha..
Mkuu wa usalama wa Taifa Kiteto, akizungumza na wanachama wa CWT Kiteto..
Kaimu mkuu wa Polisi Kiteto, Patrick Kimaro akizungumza mbele ya mkutano wa CWT Kiteto..
Kaimu mkuu wa magereza Kiteto katika mkutano na CWT Kiteto..
Wanachama wa CWT Kiteto wakifuatilia mkutano wao mkuu..
Wanachama wa CWT Kiteto wakifuatilia mkutano wao mkuu..
Wanachama wa CWT Kiteto wakifuatilia mkutano wao mkuu..
Wanachama wa CWT Kiteto wakifuatilia mkutano wao mkuu..
Wanachama wa CWT Kiteto wakifuatilia mkutano wao mkuu..
Kamati ya utendaji wa CWT Kiteto wakifuatilia kikao..
Picha ya pamoja ya kamati ya ulinzi na Uasala Kiteto na uongozi wa CWT Kiteto..
Uongozi wa CWT Kiteto katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa..
Na, MOHAMED HAMAD
WANACHAMA wa chama cha walimu Kiteto, mkoani Manyara, wamekutana ukumbi wa jengo la maendeleo ya jamii Kiteto kujadili mambo yanayowakabili katika majukumu ya kila siku kuwatumikia wananafunzi (Kusomesha)
Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mwenyekiti wa CWT Kiteto Paulo Gwacha, alimwambia mkuu wa wilaya kuwa pamoja na walimu kuwajibika katika nafasi zao bado wanachangamoto lukuki
Miongoni mwa changamoto hizo ni waalimu kufanya kazi katika mazingira magumu, kama vile uhaba wa vyumba vya madarasa, vitendeakazi, pamoja na kutolipwa haki zao kwa wakati hali inayofanya wakate tamaa
Akizungumza na walimu hao Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa, aliwataka waalimu hao kutokata tamaa dhidi ya Serikali yao akisema iko bega kwa bega na walimu hao katika kuwatumikia wananchi
Kwa upande wake katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Ndaki Stephano aliwataka waalimu hao kuwajibika ipasavyo akisema Serikali ya awamu ya tano haina mchezo katika kuwatumikia wananchi wake
Akizungumza na wanachama hao Katibu wa Chama hicho Waziri Banga aliitaka Serikali na waajiri kutumia lugha za upole katika kuwasiilisha ujumbe tofauti na ilivyo sasa kuwa watumishi wanafanya kazi kwa hofu kuhofia kutumbuliwa
"Chama kitahakikisha waalimu wanapatiwa haki zao kama kinavyoendelea kujinadi kupitia mazungumza na waajiri kuepuka malumbano,isipokuwa tunaomba viongozi wa Serikali kutumia lugha nyepesi katika kuwasilisha ujumbe"
Inaendelea..
Maoni
Chapisha Maoni