Nyanda ya malisho OLENGAPA yanufaisha wafugaji wilayani Kiteto

Wajumbe waliounda malisho ya pamoja (OLENGAPA) kifupisho cha vijiji vinne Orkitikiti, Lerug, Ngapapa na Engungwangare...

Wawakilishi wa vijiji vinne vilivyounda nyanda ya malisho ya pamoja OLENGAPA Kiteto wakifuatilia kikao..

Wawakilishi wa vijiji vinne vilivyounda nyanda ya malisho ya pamoja OLENGAPA Kiteto wakifuatilia kikao..
Mwenyekiti wa Kijiji cha Orkitikiti, Yakobo Oloisiaji akizungumza kikao cha makubaliano ya pamoja juu ya matumizi ya eneo pamoja la malisho la OLENGAPA kata za Kijungu na Lengatei

Mmoja wa Viongozi wa vijiji vilivyounda eneo la pamoja la OLENGAPA akisaini mkatapa wa pamoja wa vijiji hivyo

Baadhi ya viongozi wa vijiji vilivyounda malisho ya pamoja OLENGAPA wakiwa katika makubaliano ya pamoja ya kuwekeana mikataba ya namna ya kutumia eneo hilo

Kuwekeana saini namna ya kutumia eneo la pamoja la OLENGAPA Kiteto Manyara..






Nyanda ya malisho OLENGAPA yanufaisha wafugaji wilayani Kiteto


Na, MOHAMED HAMAD

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Uendelezaji Endelevu wa Nyanda za Malisho (SRMP), umewezesha upatikanaji wa ardhi ya Nyanda za Malisho ya (OLENGAPA) yenye ukubwa wa ekari 75,000 wilayani Kiteto

Mradi huo unalenga upatikanaji wa ardhi ya malisho kwa ajili ya ufugaji endelevu na wenye tija ili kuepusha migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

Vijiji vilivyounda nyanda hizo ni Orkitikiti, Lerug, Ngapapa na Engangongare ambavyo kwa pamoja viliwekeana mkataba wa namna bora ya kutumia eneo hilo kwa ajili ya malisho.

Boniphace Shija mtaalamu kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi akizungumza na MTANZANIA alisema Wizara itahakikisha mradi huo unakuwa na manufaa kwa vijiji hivyo akisema utapunguza migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji.

Alisema mradi huo ulioanza mwaka 2010 uko katika awamu ya tatu na mipango ya baadaye ni kuboresha maeneo ya nyanda za pamoja za malisho kama njia ya kuifanya jamii ya wafugaji kunufaika.

Mradi huo unatekelezwa kwa pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, RECONCILE ya Kenya, CARE International naTNRF.

Mengine ni NLUPC (Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi), KINNAPA na halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara na unafadhiliwa na IFAD, Irish Aid, ILRI na ILC.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Orkitikiti Mussa Olesiaji (mfugaji) alisema awali waliishi kwa amani na baada ya ongezeko la watu migogoro ilianza, kwa kushirikiana na SRMP walianzisha nyanda za malisho ya pamoja OLENGAPA

“Naiomba Serikali itusaidie kuchimba mabwawa pamoja na majosho katika eneo hili ambayo yatasaidia mifugo kutafuta maji umbali mrefu na pia kuepuka migogoro kati ya wakulima na wafugaji”alisema Mussa.

Ismail Mapori (mkulima) wa Kijiji Cha Ngapapa alisema,  mpango huo utasaidia jamii ya wakulima kuondokana na usumbufu wa mifugo kuharibu mazao shambani ambapo itakuwa inachungwa eneo maalumu.

Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Orkitikiti Jacobo Olosiaji alishukuru Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na wafadhili walioshiriki kuanzishwa nyanda za malisho akisema ni mkombozi kwa jamii hiyo.

MWISHO.


Maoni