Waziri Jafo akiwa Kiteto Manyara Tanzania kwenye ukaguzi wa barabara ya thaani ya bil 6.4
Jafo amtimua mkandarasi Kiteto
Jafo amtimua mkandarasi Kiteto
Na, MOHAMED HAMAD
WAZIRI wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Selemani Jafo, ameisimamisha kazi kampuni ya Maginga inayotengeneza barabara kwa kutoendana na masharti ya mkataba waliyopewa Wilayani Kiteto.
Barabara hiyo ina urefu wa km 88.1 kutoka kata ya Namelock hadi kata ya Sunya, ambayo inagharimu bil 6.4 kwa msaada wa watu wa Marekani.
Alimtaka mkandarasi huyo kukutana na meneja wa Tarura Wilaya Mhandisi Gerald Matindi ndani ya siku tano kufanya tathmini ya kisi cha kazi iliyofanyika na kulipwa stahili yake kinyume chake atafikishwa katika vyombo vya kisheria.
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara Emmanuel Papian (CCM) mbele ya Waziri Jafo alimshukuru kwa hatua hiyo akisema kasi hiyo itasaidia Tanzainia kupiga hatua mbele zaidi.
Alisema Kampuni hiyo inafanya kazi chini ya kiwango kutokana na kulindwa na Meneja wa Tarura Wilaya ambaye ni rafiki yake akiomba hatua za namna hiyo ziwe zinachukuliwa ili iwe fundisho kwa maeneo mengine kama hayo
Meneja wa Tarura wilaya mhandisi Gerald Matindi alisema mkandarasi huyo ameshindwa kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa, kwani amefanya kazi kilometa kumi na saba tu kati ya kilometa 44, tangu ameanza kazi hiyo tarehe 17/06/2017.
Mtendaji mkuu wa Tarura Tanzania mhandisi Victor Seif alisema wakandarasi wa aina hiyo kama watakuja kuomba kazi hawana nafasi na ikitokea kwamba wameleta vigezo ambavyo sio vya kweli wakapewa kazi Tarura itasitisha mikataba yao. alisema Mhandisi Seif
Abasi Famau mwananchi wilayani Kiteto alisema pamoja na Serikali kuwa na nia njema, iangalie namna ya kuboresha wakala huyo wa barabaraTarura ili aweze kukutana na wanufaika wa barabara hizo.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni