Kiteto yaongeza wasiojua kusoma na kuandika

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Fadhili Alekzander, akifafanua jambo kwenye ripoti ya kupima uwezo watoto wa miaka 7-17 wa kusoma kiingereza, kiswahili na kufanya hesabu Wilayani Kiteto Manyara cchini ya UWEZO TANZANIA


Asia Lambariti kutoka UWEZO TANZANIA  akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa ripoti Kiteto ya UWEZO iliyofanyika Kiteto..


Diwani wa kata ya Kibaya, Kassim Msonde alifafanua jambo mjini Kibaya kwenye uzinduzi wa taarifa ya kupima uwezo wa watoto iliyofanyika 2015
Mwadawa Ally akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya UWEZO mjini Kibaya..


Abasi Famau akisoma taarifa ya shughuli za UWEZO zilizofanyika Kiteto 


Mbwana Jumaa akipokea cheti baada ya kukamilisha taarifa ya UWEZO mjini Kiteto Manyara..
Mwadawa Ally kiongozi wa shirika la KIWOCOA na mwakilishi wa mkuu wa Wilaya wakifuatilia jambo kwenye uzinduzi..


Asia Lembariti w UWEZO katikati na Joseph Mwaleba Afisa maendeleo na Bi Mwakibete wakifuatilia taarifa ya UWEZO mjini Kibaya..
Abasi Famau na Aimbile Ali wakifuatilia taarifa ya UWEZO mjini Kibaya..



Uzinduzi wa taarifa ya UWEZO Kiteto..


Picha ya pamoja baada ya kuzinduzi wa ripoti ya uwezo Kiteto Manyara..



Wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu Kiteto waongezeka 

Na, MOHAMED HAMAD
IDADI ya watoto wasiojua kusoma, kuhesabu na kuandika kwa kiwango cha darasa la saba wilayani Kiteto mkoani Manyara imeongezeka na kufikia 28% katika utafiti uliofanyika 2015

Kipindi cha miaka sita iliyopita, tathmini ya uwezo inaonyesha kuwa watoto hawafanyi vizuri katika katika masomo yao kwa kiwango kinachotakiwa kutokana na sababu mbalimbali 

Moja ya sababu hizo ni pamoja na kutogawanywa kwa uwiano sahihi wa rasilimali za nchi vilivyo hivyo baadhi ya maeneo kuonekana kuwa na ufaulu mzuri na mengine mbaya 

Sababu zingine ni mahudhurio hafiu ya waalimu na wanafunzi darsani,hali inayosababisha wanafunzi kukosa haki yao ya kimsingi ya kujifunza wanapokuwa shuleni 

Pia ukosefu wa chakula shuleni kwa baadhi ya shule na kusababisha wanafunzi kutofanya vyema pamoja na uhaba wa miundombinu ya kielimu kama vile madarasa, nyumba za waalimu na matundu ya vyoo

Wakiwasilisha mchango yao baada ya ripoti hiyo wadau hao wamesema pamoja na waalimu kutakiwa kuongeza bidii katika ufundishaji Serikali nayo inatakiwa kuwapa stahili zao ili waweze kutimiza wajibu wao

Mwisho


Maoni