Kiteto yatekeleza kauli mbiu ya kukuza uchumi wa viwanda

Kiteto yatekeleza kauli mbiu ya kukuza uchumi wa viwanda

                                                                                                                                    
                 Kiongozi wa mbio za mwenge ndugu Amour Hamad Amour akisikiliza maelezo jinsi kiwanda cha Kwadelo Sunflower and Super kinavyofanya kazi kabla ya uzinduzi kipo kata ya Matui Aliyesimama kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Tumaini Magessa
                                                                                                                                                                
                                                                                                                                                                 
               Jengo la wodi ya wanawake na watoto lililozinduliwa na   Mwenge  wa uhuru katika kata ya Matui .
Jengo la madarasa yaliyozinduliwa na mwenge katika shule ya sekondari Engusero.

           Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour akikagua darasa lililozinduliwa na mwenge katika shule ya sekondari Engusero katika kata ya Engusero.Walioambatana nae ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Tumaini Magessa,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kiteto Ndg. Tamim Kambona na maafisa wengine wa serikali wilayani Kiteto.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour akifungua mradi wa maji katika kata ya Kaloleni.

Kwa Hisani ya tofuti ya halm ya Kiteto

Wilaya ya Kiteto imetekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka  2017 ambayo ni shiriki  katika kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu, kwa kuanzisha  kiwanda cha kukamua alizeti na kusaga mahindi.
Kiwanda hicho kilichopo kata ya  Matui  ni miongoni mwa miradi minne iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru wilayani kiteto yenye thamani ya shilingi mil. 400,050,000.
Miradi mingine iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru  ni madarasa  mawili  yaliyojengwa katika shule ya sekondari  Engusero iliyopo  katika kata ya Engusero .Mradi huo wa madarasa una thamani ya shilingi 26,740,120,ambapo halmashauri imechangia shilingi 865,000.
Kikundi cha vijana Kaloleni kilizinduliwa, kikiwa na lengo la kuwawezesha vijana kuendesha shughuli za kiuchumi na kukuza kipato cha kila kijana,na kuna miradi mbali mbali kama ufugaji kuku  chotara, uuzaji wa vifaranga na mayai, kilimo cha mbogamboga, biashara ya bodaboda na VIKOBA
Miradi yote hiyo ina thamani ya shilingi 8,200,000 ,ambapo  halmashauri  ya wilaya  ilikipatia kikundi hicho mkopo wa shilingi  2,000,000,fedha  ambayo  ilitumika  kununua  pikipiki, ambazo zinawawezesha vijana hao kupata marejesho  na kuendesha shughuli nyingine za kikundi.
 Mradi mwingine uliozinduliwa ni kampeni  ya kutokomeza  malaria, wilaya ya Kiteto ilianzisha kikundi  cha kupambana na kutokomeza  ugonjwa  wa malaria.Mradi huo una thamani ya shilingi 500,000,ambapo fedha hizo zilitolewa na halmashauri .
Mradi wa ujenzi wa jengo la wodi ya wanawake  na watoto  umewekewa jiwe la msingi.Mradi huo  wa wodi upo katika kata  ya matui na una thamani ya shilingi 37,796,000,  halmashauri ya wilaya ya Kiteto imechangia shilingi 20,246,000 .
Sambamba na hayo, mradi wa maji ulifunguliwa . Mradi huo uko katika kata ya Kaloleni na  una thamani ya shilingi 255,915,500, kati ya fedha hizo ,halmashauri imechangia shilingi  5,000,000.
Katika  hatua  nyingine  miradi miwili ilikaguliwa ambayo ni kikundi cha wanawake, lengo la kuwawezesha wanawake  kuendesha shughuli za kiuchumi na kukuza kipato kwa kufuma mashuka ya kimasai ushanga ,kutengeneza shanga,hereni na mikufu ,usindikaji vyakula , uuzaji wa bidhaa mbalimbali kama sukari ,mchele na sabuni  na VICOBA. Miradi yote  hiyo ya kikundi cha wanawake ina  thamani ya shilingi 10,500,000. 
Mradi mwingine uliokaguliwa ni mradi wa utunzaji wa mazingira, ambapo  zoezi la upandaji miti  katika eneo la shule ya Sekondari  Engusero lenye ukubwa wa ekari 2.5 lilifanyika ikiwa ni sehemu ya utunzaji mazingira katika wilaya ya Kiteto. Mradi huo una thamani ya shilingi 1,420,000, ambapo halmashauri imechangia shilingi 160,000.
Mwenge wa uhuru umepokelewa wilayani Kiteto na mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magesa,  ambapo umepitia katika tarafa  tatu,kata saba ,vijiji kumi na tano  na kukimbizwa umbali wa kilometa 90 kutoka eneo la mapokezi hadi eneo la mkesha.Jumla ya miradi 8 imepitiwa na mwenge wa uhuru , thamani  ya  miradi yote  iliyopitiwa ni shilingi za kitanzania 750,571,120, ambapo wadau wa maendeleo wamechangia shilingi 17,210,000 , Jamii shilingi 444,900,00, halmashauri ya  wilaya ya Kiteto shilingi 28,771,000 na serikali kuu shilingi 259,690,120.

Maoni