LHRC waungana na wadu wengine kupinga ukatili

Wadau wa ngazi ya jamii wilaya za Kiteto, Mbulu, Hanang, na Babati wakiunga mkono siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia, mjini Kibaya..Kiteto ambapo mkoa wa Manyara unaongoza kwa ukeketaji wa watoto wakike hapa Nchini..
Wadau wa sheria wilaya za Kiteto, Babati, Hanang na Mbulu wakiwa mjini Kibaya Kiteto baada ya kupata elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na ukeketaji chini ya Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC.
Wakili Naemy Silayo wa LHRC Dar..akifafanua jambo kwenye mafunzo ya siku mbili kuhusu ukeketaji ambapo mkoa wa Manyara Kitaifa unaongoza..
Mwenyekiti wa mafunzo Mashaka Saidi Fundi alifafanua jambo mbele ya wadau wa sheria mjini KIbaya Kiteto ambao chini ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wakipatiwa mafunzo ya siku mbili kuhusu ukatili wa kijinsia..
Rodrck Marro mwanasheria akifuatilia mafunzo ..

Wadau wa sheria toka wilaya za Kiteto, Babati, Hanang na Mbulu wakifuatiilia masomo ya ukatili wa kijinsia mjini Kibaya Kiteto Manyara..
Mmoja wa washiriki Mwl Rehema mbele ya darasa akieleza wajumbe kazi za shirika la ECAN(T) linalofanya kazi ya kuzuia ukatili kwa watoto nchini Tanzania..
Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Kiteto Elimo Masawe kulia akifafanua jambo mbele ya wadau wa sheria kutoka wilaya nne za mkoa wa Manyara..ambao hawapo pichani kushoto ni Bruno Bongole hakimu mahakama ya mwanzo kwenye mafunzo ya siku mbili chini ya LHRC yaliyofanyika mjini Kibaya Kiteto Manyara..
Hakimu Elimo Massawe wa mahakama ya wilaya Kiteto akifafanyua jambo, kulia na Wakili Naemy Sillayo wa LHRC Dar..na kushoto ni Buno Bongole wa mahakama ya mwanzo Kibaya..


NA. MOHAMED HAMAD
KITUO cha sheri na haki za Binadamu LHRC kimefanya mafunzo ya siku kwa wadau wa ngazi ya jamii kutoka wilaya za Kiteto, Hanang, Babati na Mbulu kuhusu ukatili wa kijinsia ambapo Manyara imedaiwa kuongoza hapa nchini..

Wadau hao ni walimu, wauguzi, wazee wa mila,watendaji wa kata na vijiji, wasaidizi wa kisheria, viongozi wa dini, maafisa ustawi wa jamii, na wanasheria kutoka wilaya hizo ambapo mafunzo hayo yalifanyika mjini Kibaya..

Mada zilizotolewa ni ukatili wa kijinsia na Ukeketaji, ambapo kwa pamoja wameungana na wananchi katika siku 16 za kupinga vitendo hivyo ambapo kwa mkoa wa Manyara umedaiwa kuongoza kwa ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake ambapo kati wa wasichana 100, mkoani humo 58 wanakeketwa..

Akizungumza na wadau hao Bi. Naemy Sillayo mratibu wa kitego cha jinsia na watoto katika kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC amesema jamii zinapaswa kubadilika na kuondokana na tabia za kukumbatia mila na tamaduni kandamizi ili mtu aweze kushiriki kikamilifu shughuli za kijami, Kiuchumi na kisiasa..

Makundi hayo yalikubaliana kwa pamoja kutokomeza ukatili yakiongozwa na kundi la wazee wa mila ambapo kwa pamoja waliapa kusimamia sheria ili kufikia malengo tarajiwa

ya jamii...

Akizungumza mbele ya washiriki hao, Elimo Masawe hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya aliwataka wasaidizi hao kuacha kuwapa matumaii ya uongo wateja wao wanapowasaidi na badala yake wametakiwa kusimamia haki

Kwa upande wake Rodrick Maro (wakili) LHRC akiwasilisha somo la ukatili wa kijinsia alisema chanzo cha ukatili huo kukosema na elimu na kuendekeza mila na imani potofu ndani ya jamii na kuonya kuwa sheria itachukua mkondo wake

Mwenyekiti wa semina hiyo Mashaka Saidi Fundi, aliwahakikishia mawakili wa LHRC kuwa elimu hiyo itakuwa na manufa kwa wananchi hao kwani baada ya kumalizika kila mjumbe ataelekea kwake tena kwa hali ya kutaka kuimarisha utawala katika ngazi husika..

Mwisho

Maoni