Madiwani Kiteto wataka watumishi kuwajibika

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel, akifafanua jambo kikao cha madiwani robo ya tatu ya mwaka Kiteto 2017..

Diwani Mwasigwa Kimosa, akiwasilisha taarifa mbele ya kikao cha baraza la madiwani Kiteto Manyara Tanzania..


Mhe Ng'ungu diwani wa kata ya Matui Kiteto Manyara akitoa taarifa ya kata mbele ya baraza la madiwani, Kiteto Manyara, Tanzania...


Diwani wa kata ya Sunya Mussa Briton akitoa taarifa ya kata kwenye kikao cha madiwani Kiteto.. Manyara Tanzania


Diwani Rehema Cheleleu akichangia kwenye kikao cha madiwani Kiteto Manyara Tanzania..2017


Paulo Tunyoni Diwani wa Kata ya Partimbo akifafanua jambo kikao cha madiwani Kiteto Manyara..

Diwani wa kata ya Ndedo akifafanua jambo kikao cha madiwani Kiteto Manyara 2017



Emanuel Mwagala kaimu DED Kiteto akifafanua jambo kikao cha madiwani 2017 ..

Wakuu wa Idara Kiteto wakifuatilia jambo kwenye kikao cha baraza la madiwani 2017..


NA, MOHAMED HAMAD
MADIWANI wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wamewaonya baadhi ya watumishi wa Serikali kwa kutofanya kazi kama mikataba yao inavyoelekeza

Wakizungumza kwenye kikao cha madiwani cha hivi karibuni, wamesema baadhi ya watumishi wamekuwa kero, hawahitaji kuwatumikia wananchi mpaka wapatiwe fedha za ziara ili waweze kufika maeneo yao

Akizungumza mbele ya kikao hicho, Christopher Parmet alisema amekuwa mhanga wa kwanza kama kiongozi kutakiwa fedha na mtumishi wa Serikali ili apate ushauri katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

"Mhe mwenyekiti tunaelekea wapi mbona fedha inaonekana kuwekwa mbele zaidi kuliko huduma kwa watumisi wetu wa Serikali, tunapohitaji ushauri hatupati wakati wanalipwa mishahara na Serikali?alihoji Diwani Parmet.

Akifafanua hayo Parmeti alisema katika hali isiyotazamiwa baada ya kuomba msaada wa kitaalamu kutoka idara ya ujenzi aliambiwa mtumishi hawezi kwenda mpaka apatiwe fedha ili afike katika eneo husika kwa ushauri huo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel alionyesha kukerwa na kitendo hicho kisha kutoa onyo kali huku akisema hatua kali zitachukuliwa kwa watumisi wengine kama hao ambao hawatowajibika katika nafasi zao.

Kwa Upande wake Emmanuel Mwagala kaimu mkurugenzi mtendaji wa halamashauri alisema, amelipokea na kwamba atachukua hatua kali zinazostahili kwa watumishi wanaokiuka utaraibu wao wa kazi tofauti na mikataba yao.

mwisho..

Maoni