Mbunge amtonya waziri Jaffo kuwa amedanganywa


Waziri wa Nchi Tawala za mikoa na Serikali za mitaa, Selemani Jaffo (MB) akizungumza na viogozi wa Kiteto, akiwa katika ukaguzi wa mradi wa barabara inayoanzia kata ya Namelock hadi kata ya Sunya km 88 ya thamani ya bil 6.4 kulia ni Emmanuel Papian (MB) CCM na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa  



Waziri wa Nchi Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Selemani Jaffo akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya ya Kiteto (ofisi) la ghorofa moja, ambapo kwa sasa imedaiwa Serikali inachelewesha mradi huo kwa kutotoa fedha kwa mkandarasi 

Waziri wa Nchi Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Selemani Jaffo akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya ya Kiteto (ofisi) la ghorofa moja

Waziri Jaffo mwenye suti nyeusi tai nyekundu akitafakari juu ya mradi wa ujenzi wa barabara unaodaiwa kujengwa chini ya kiwango 

Waziri Jaffo amepata fursa ya kuitembelea shulea ya sekondari ya Engusero..

Picha ya pamoja Waziri Jaffo na Wanafunzi wa Engusero Sekondari..
Watumishi wa Afya Kiteto wakisalimiana na Waziri Jaffo..

Waziri Jaffo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Engusero Kiteto Manyara 




Waziri Jaffo akiagana na viongozi Kiteto akiwepo Kaimu OCD Kiteto Patrick Kimaro, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa, na Mbunge wa Jimbo la Kiteto Emmanuel Papian..





Mbunge amtonya waziri Jaffo kuwa amedanganywa

Na, MOHAMED HAMAD
MBUNGE wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Emmanuel Papiani (CCM), amemwomba Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo kuunda kikosi kazi kuchunguza mradi wa ujenzi wa barabara unaogharimu bil 6.4 kuwa uko chini ya kiwango.

Mradi huo unatekelezwa chini ya unafadhiliwa na watu wa Marekani (USAID) wenye urefu wa km 88  kuanzia kata ya Namelock hadi kata ya Sunya ambao unakusudiwa kunufaisha wananchi hao

" Mhe Waziri wewe sio mtaalamu sote ni wanasiasa.. hapa umedanganywa na meneja wa Tarura, angalia vifusi,.. linganisha na kazi inayofanywa na mkandarasi kutoka Sunya kuja huku Namelock, mimi nimekataa" alisema Mbunge Papiani

Alisema mkandarasi anayejenga barabara hiyo yuko chini ya kiwango na ni rafiki ya Meneja wa Tarura hawezi kumchukulia hatua, hivyo kama mwakilishi wa wananchi siko tayari kuona hayo yakiendelea huku wananchi wakitaabika

Akizungumza mbele ya Waziri Jaffo Meneja wa Tarura wilaya Mhandisi Gerald Matindi alisema mkandarasi huyo ameomba kupewa siku saba afanye kazi, awali  alifanya vizuri baada ya kupewa siku 14 hivyo yuko chini ya uangalizi

Hata hivyo Waziri Jaffo alionyesha hofu katika mradi huo na kumtaka Meneja wa Tarura kuchukua hatua zinazostahili kwa mkandarasi huyo huku akiahidi kurejea tena Kiteto tarehe 17 mwezi ujao ili kuona kinachoendelea kwani mradi huo unatumia gharama kubwa

"Kama sasa mkandarasi yuko nyuma ya muda na utendaji wake wa kazi ni mpaka asukumwea..huyu hata akiifanya hiyo kazi itakuwa chini ya kiwango hivyo atafanya wananchi wasinufaike na mradi huo"

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Engusero Waziri Jaffo alisema, Serikali ya awamu ya tano imelenga kutatua kero za wananchi kwa kutoona mwananchi wakilalamika 

Kiteto tumewapa mil 400 kwaajili ya uboreshaji wa kituo cha Afya Sunya, na tutajenga mabweni mawili ya Sekondari ya Engusero, pamoja na kuongeza matundu ya vyoo sambamba na kumpatia fedha mkandarasi anayeendelea na mradi wa ujenzi wa jengo la halmashauri la ghorofa moja.

mwisho

Maoni