WAZIRI Jaffo atishia kutumbua wawili Kiteto



Waziri wa Nchi Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo (MB) akimsikiliza Meneja wa Tarura Mhandisi Matindi akifafanua ujenzi wa barabara kutoka kata ya Namelock mpaka Sunya km 88 Kiteto Manyara Tanzania ya thamani ya Bil 6.4



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Miraa, Selemani Jaffo (MB) akionyesha hali ya kutorizika na ujenzi wa barabara ya km 88 kutoka kata ya Namelock hadi Kata ya Sunya Wilayani Kiteto inayojengwa kwa thamani ya Bil 6.4

Bango linaloonyesha wahusika katika ujenzi wa mradi wa barabara ya km 81 kuanzis Namelock hadi Synya ya thamani ya bil 6.4

Waziri wa Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akizungumza na watumishi wa Serikali ya Kiteto katika ukaguzi wa miradi yupo Mkuu wa Wilaya Tumaini Magessa na Mbunge wa Jimbo Emmanuel Papiani (CCM)

Picha ya pamoja Waziri Jaffo na wanafunzi wa sekondari ya Engusero Kiteto Manyara

 Waziri Jaffo akielekea kwenye mkutano wa wananchi katika wa kata ya Engusero Kiteto Manyara Tanzania

Waziri Jaffo akihutubia wananchi wa Kijiji cha Engusero Kiteto

Wananchi wa Kijiji cha Engusero wakifuatilia mkutano wa Waziri Jaffo

Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa Waziri Jaffo Kiteto Manyara

Uongozi wa Wilaya ya Kiteto ukimwaga Waziri Jaffo baada ya kuhitimisha ziara ya siku moja wilayani humo



NA MOHAMED HAMAD

WAZIRI wa Nchi Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo, amemaliza ziara yake wilayani Kiteto mkoani Manyara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa ofisi za Serikali ghorofa moja, na kuahidi kuwa Serikali itatimiza wajibu wake.

Waziri Jaffo amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa kuwa jengo hilo linasuasua na huenda likamalizika nje ya muda kutokana na Serikali kutotoa fedha kwa wakati hivyo kumfanya mkandarasi kutotimiza wajibu wake ipasavyo.

Akikagua ujenzi huo Waziri Jaffo alisema, Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha kuwa inawatumikia wananchi kikamilifu sambamba na kupunguza kero zinazowakabili akisema kwa sasa wataipatia halmashauri hiyo fedha ili kukamilisha ujenzi huo

"Sina shaka na huyu mkandarasi, nimeona kazi zake maeneo mengi hapa nchini kuwa ni nzuri hivyo niseme tu kuwa Serikali pamoja na kuchelewa kutoa fedha nitaenda kusukuma mambo haya ili fedha hizo zije kwa wakati naye akamilishe kazi".

Wakati huo Mbunge wa Jimbo la Kiteto Emmanuel Papian alimtaka waziri Jaffo kuunda timu yake kuchunguza ujenzi wa barabara inayoanzia kata ya Namelock hadi Sunya km 88 ya thamani ya Bil. 6.4 kuwa inajengwa chini ya kiwango.

Alisema Meneja wa Tarura wilaya, ambaye ni Mhandisi Gerald Matindi amekuwa tatizo kutosimamia kazi hiyo kikamilifu na kumkumbatia mkandarasi ambaye anaonekana kuzembea kazini kwa kuwa ni rafiki yake hivyo kama mwakilishi wa wananchi hawezi kumvumilia kuona hayo yakitendeka

Meneja wa Tarura Wilaya mhandisi Gerald Matindi alimwomba Waziri Jaffo kumpa siku 7 mkandarasi huyo kwani aliomba siku 14 za kufanya kazi na kwamba akishindwa ndipo achukuliwe hatua

Akizungumza katika maeneo hayo Waziri Jaffo alionyesha hofu yake katika utekelezaji wa mradi huo alisema kama anafanya kazi kchini ya kiwango tena kwa usimamizi hata akipewa siku hizo hatoweza kufanikiwa

"Meneja wa Tarura..kabla sijakutumbua anza kumtumbua huyu mkandarasi..mimi nitakuja tarehe 17 mwezi ujao, nikikuta hali hii sitokubakisha, siwezi kubaliana na kasi hii,..wakati haya yanafanyika ulikuwa wapi?alihoji Waziri Jaffo


Waziri Jaffo alifika shule ya Sekondari Engusero ya kidato cha kwanza hadi cha sita na kuahidi kuwa atahakikisha Serikali inaleta fedha kwaajili ya majengo mawili ya kulala wanafunzi (mabweni), jengo la kulia chakula, pamoja na vyoo.

Katika mkutano na wananchi wa Kijiji cha Engusero Waziri Jaffo aliulizwa maswali liliwepo la halm kutotoa 20% za vijiji hali inayofanya vijiji vingi kushindwa kujiendesha kwa kukosa mapato baada ya kuchukuliwa na halmashauri.

Akijibu swali hilo kaimu mweka hazina wa Wilaya ya Kiteto Shigi Thomas alisema anamshangaa mwananchi huo kuuliza wakati wanaletewa fedha za maendeleo, huku mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Lairumbe Molel akisema Serikali imejenga mabweni kwa fedha nyingi kuliko wanazouliza, na kuongezewa na Diwani wa kata hiyo Mbulunyuku kuwa Serikali inakusanya fedha  vijijini na kwamba marejesho ni miradi inayoletwa

Waziri Jaffo akaulizwa.

DT una muda gani na kazi hii?

Jibu miaka minne.

Swali unakaimu au wewe ndio DT mwenyewe

Jibu nimekaimu mh Waziri..

Haya kaa chini basi maana ungekuwa DT leo ningekutumbua muda huu.. Serikali ya awami ya tano haitaji ubabaishaji kama huu, Mhe Rais ametuagiza tuhakikishe kuwa tunajibu kero za wananchi na kuacha ubabaishaji

Hata hivyo majibu hayo hayakumridhisha Waziri Jaffo alisema hoja ya mwananchi Binaisa Selemani kutaka 20% haijajibiwa na kumtaka Mkurugenzi na madiwani kutenga asilimia 20% za kila kijiji na kuwapa ili ziweze kufanya kazi ya kuendesha ofisi zao.

Mwisho





Maoni