Mbwana Juma (kushoto), Mohamed Hamad (katikati) na Abasi Famau kulia..
Kituo cha habari Kiteto.
WILAYA ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara,
ilizinduliwa mwaka 1974, ikiwa na makabila makuu matao ambayo ni waburunge, wamaasai,
wagogo, warangi na wanguu.
Wilaya ina ukubwa wa km za mraba elfu 16,885 yenye
idadi ya watu 152,000 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, na
kwamba shughuli kuu za uchumi ni kilimo na mifugo.
Harakati za vyombo vya habari ni muhimu kwaajili ya kuharakisha
shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii hivyo wajibu wetu ni kuhabarisha, kuelimisha
na kuburudisha.
Kuanzishwa kwa kituo cha habari ni wazo lililotokana
na wadau na wanahabari mjini Kibaya ambao walihitaji hasa makundi yaliyopo
pembezoni (inclusive groups)
Kwa kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,
waanzilishi wa chombo hiki ni Abasi Famau (mdau), Mohamed Hamad (mwandishi) na
Mbwana Juma (mwandishi).
Katika jitihada za kupashana habari tumefungua ofisi
katika jengo la maendeleo ya jamii Kibaya, (Community center) ambayo wakati
wote tunapatikana.
Lengo ni kutoa habari za wananchi kwa ukaribu na kwa
wakati kwa kiwango stahili ili waweze kufikia malengo tarajiwa ambayo ni
maendeleo ya pamoja.
HUDUMA
ZINAZOTOLEWA.
Ni kutolewa habari kwenye vyombo mbalibali kama
vile, TV, REDIO, MAGAZETI pamoja na mitandao mengine ya kijamii iliyopo ndani
ya nchi ya Tanzania
Wadau wa habari ambao ni mamlaka za Serikali,
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, idara mbalimbali za serikali za mitaa,
taasisi za umma, taasisi binafsi na taasisi za kidini zinakaribishwa.
Kwa mawasilian zaidi waweza kuwasiliana nasi kwa
kupiga,
Simu Na. 0787 055 080), 0656
816 825 0782 867 576 Au
Imeandaliwa
na
Mohamed Hamad
MRATIBU WA KITUO CHA
HABARI KITETO
MANYARA.
Maoni
Chapisha Maoni