NAIBU WAZIRI MADINI
STANLAUS NYONGO AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA NYAKABALE.
NAIBU WAZIRI, STANSLAUS
NYONGO, AKISISITIZA JAMBO..
NAIBU WAZIRI AKISHIRIKI
SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MDOGO..
NAIBU WAZIRI AKIPATA
MAELEZO YA WACHIMBAJI WADOGO..
NAIBU WAZIRI AKIMSIKILIZA PILI MWALUKO, ANAEFANYA KAZI YA
UCHIMBAJI WA MADINI..
GGM watakiwa kuheshimu wananchi..
Na, Merina Makasi
NAIBU waziri wa madini, Stanslaus Nyongo, amesema Serikali
ya awamu ya tano haiko tayali kuona wananchi wakilalamika na badala yake itahakikisha
inaondoa manung’uniko hayo.
Baadhi ya
wananchi wamekuwa na tabia ya kushuhudia dhulma ikitendeka katika maeneo yao bila kukemea, na kudai kamwe Serikali ya awamu wa tano haitalifumbia macho.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyakabale Mkoani Geita walikuwa wakiulalamikia mgodi wa gold mine (GGM) alisema Serikali imesikia kilio hicho na itakifanyia kazi.
“Tukikaa kwenye viyoyozi hatuambiwi ukweli na wamiliki wa migodi
lakini tunapo fika katika maeneo husika tunapata ukweli , unakuta mtu kazaliwa
hapo kakulia hapo amejenga ana watoto halafu anaondolewa huo ni ukatili”alisema
waziri huyo.
Aliwataka watu hao wa mgodi kuwalipa wananchi hao ama waondoke wao na
kuwaachia eneo lao waendelee kuchimba madini na sio kuwazuia akisema, madini ni
neema sio balaa hivyo yasiwanyanyase wahusika.
Akitoa malalamiko mbele ya Naibu Waziri , Joseph Kihengu (mwananchi)
alisema, wanaulaumu uongozi wa serikali iliyomaliza muda wake kwa kubinafsisha
mgodi huo kwa watu tofauti bila wao kujua.
Alisema wana imani na serikali ya awamu ya tano, hivyo iwatazame kwa jicho la huruma wananchi wa kijiji cha Nyakabele ili wajue hatima ya maeneo yao ambayo yapo ndani ya bikoni
mgodi wa GGM.
Katika hatua nyingine akina mama wanyakabale wakiwakilishwa na
Godliva Mgini waliutupia lawama uongozi wa mgodi huo kuwataka kuanzisha kikundi cha Baraka baada ya kuwaahidi kuwawezesha
kuanzisha mradi wa ufungaji wa nguruwe 100.
Akina mama hao waliambiwa wasombe mawe pamoja na kukamilisha ujenzi kwa gharama ya shilingi laki nane bila mafanikio jambo ambalo liliwagharimu muda na pesa nyingi.
Makamu wa Rais wa mgodi wa GGM Bw. Saimon Shayo
akisema wanatambua majirani za na baadhi ya maneno mengine yanafahamika
mengine ni mageni hivyo hekima itatumika.
Aidha alisema kuna baadhi ya watu wa nyakabale vigingi vyao vipo
ndani ya mgodi kuna watu wana haki ya umiliki wa ardhi kisheria akidai jitihada
zilizopo kuangalia namna ya kutatua tatizo kwa pamoja.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni