Waziri aonya watoroshaji madini Geita..
Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri Wa Madini Stanlaus Nyongo,
amekea tabia ya baadhi ya watendaji waliopo katika viwanja vya ndege kukosa uzalendo na kutakiwa kufanya kazi kwa weledi ili
kulinda rasilimali za Taifa.
Akiwa katika ziara mjini Geita kufatia taarifa za mtanzania
kukamtwa na kilo 32 za madini aina ya dhahabu ambayo yamesafirishwa kupitia
uwanja wa ndege wa Mwanza, alionya na kuwataka watanzania kuwa wazalendo.
Mhe. Nyongo alisema, utoroshwaji wa madini hayo unaofanyika
nchini kinyume cha sheria na haukubaliki na kuvitaka vyombo vya ulinzi na
usalama kuthibiti kupitia viwanja vya ndege hasa kiwanja cha Mwanza.
"Tunaangalia namna bora ya kuthibiti utoroshwaji wa Madini.. tukithibiti
yatasadia kuinua uchumi wa nchi yeyu kwa kiwango kikubwa, kinachofanyika sasa
hakikubaliki..’’ Alisema mhe. Nyongo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robart Gabriel, amemuomba Naibu Waziri wa
Madini Mhe. Stanslus Nyongo kuundwa kwa kamati maalumu ya kuchunguza kwa
kina utoroshwaji wa madini hayo.
Aliekamatwa uwanja wa ndege wa Nairobi
atakuwa alitoka Mkoa wa Geita ambao una dhahabu na uwepo wa madini
hayo unatokana na uwepo wa miamba mikubwa iliyobeba dhahabu.
Aidha alisema uwepo wa mianya ya utoroshaji
wa madini una sababisha kuikosesha mapato stahiki serikali kutokana na shughuli
za usagaji na uoshaji (uchenjuaji) ambazo zimekuwa zikifanyika pasipo uwepo wa
sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Geita amemuomba Naibu Waziri wa Madini kuwa,
Serikali iangalia ofisi ya madini Geita kwa ukaribu pamoja na kuiboresha
na kuipatia vitendea kazi vya kutosha.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni