Mmoja wa wamiliki wa mgodi
wa Nyarugusu, akipokea maagizo kutoka kwa Naibu Waziri wa Madini
Wananchi wakifungua njia waliyokuwa wameifunga awali..
Naibu waziri akiangalia mambwawa yaliyoleta madhara kwa
wananchi
Waziri ataka wananchi walipwe fidia ya mil 202
Na, Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa madini, Stanslaus Nyongo, amewataka wamiliki wa
mgodi wa Nyarugusu Mine Company, kulipa fidia ya shilingi million 202, wanazodaiwa na wakazi 123 wa kijiji cha Nyarugusu.
Serikali kupitia wizara ya madini wanayo dhamana, kutoa vibali
ama kuwanyang’anya wamiliki leseni ya uchimbaji wanaokaidi na
kukiuka sheria na taratibu za nchi.
Katika eneo hilo wawekezaji hao ambao ni wazungu, wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu, wanadaiwa shilingi
mil 202 kama fidia ya wananchi 123 baada ya kupata madhara kufuatia kazi hiyo ya uchimbaji wa madini.
Naibu waziri huyo alitoa agizo hilo baada ya wakazi
hao kufunga njia ya kuingia Mgodini, kufuatia madai hayo ambayo wamekuwa
wakiyadai kwa muda mrefu bila mafanikio.
Awali wakiwasilisha malalamiko yao baada ya wananchi hao kuzuia
njia, kiongozi wa wahanga hao, Shardiraki Mashaka, alisema miezi 4 iliyopita
walikosa chakula baada mashamba yao kuingiliwa na maji yenye sumu na kuharibu
mazao hali iliyofanya wakose chakula na kuwasababisha njaa.
‘’Kuzuia njia ya kuingia mgodini mmefanya sawa kwa
sababu mnadai haki yenu, nilimtafuta sana huyu mzungu toka jana lakini nina taarifa
kuwa polisi wamemakamata tayari’’ alisema Waziri Nyongo
Naye Pili Ramadhani, (mhanga) anasema walishirikiana na serikali
kufanya tathimini ya uharibifu uliotokea kwenye mashamba yao na baadae
wakaambiwa wafungue akaunti benki kwa ajili malipo yao lakini cha
kushangaza hawakupewa
Alisema mmiliki wa mgodi aliwajibu kuwa katika madai yao wamefanya
udanganyifu kuongeza maeneo na kuingiza watu ambao hawastaili kulipwa jambo
ambalo sio kweli.
‘’Mhe naibu waziri tumefikia aamuzi wa kuifunga njia ya
kuingilia mgodini baada ya kuambiwa tutalipwa fidia lakini mpaka sasa umefika
hapa hakuna lililofanyika na uongozi wa mgodi zaidi ya kutuambia tufungue
akaunti kwa ajili ya malipo’’ alisema mwananchi huyo.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Nyarugusu alisema tangu November
mwaka jana mashamba yao yalingiliwa na matope yenye sumu na serikali ikafanya jitihada
kuzungumza na uongozi wa mgodi wa TFC ili walipe fidia.
Alisema tatizo ilililotokea
baada ya wamiliki wa mgodi kuleta barua kuwa hawawezi kutoa fidia mpaka wajiridhishe
kutokana na vipengele vyao hapo ndio lililipokuja tatizo.
Akizungumza na mmoja wa mmiliki wa mgodi huo ambae hakutaja jila
lake, alisema Naibu Waziri amewataka kwa kushilikiana na mkuu wa wilaya ya
Geita kumaliza tatizo ilo ndani ya wiki moja kulipa madai yao tofauti na hivyo Wizara
watachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mgodi Uuho wa Nyarugusu.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni