Alichonena Mkapa ni sahihi

Naunga mkono hoja ya rais mstaafu ndg. Benjamin Mkapa juu ya kufanyika mjadala wa kitaifa kuhusu kudorola kwa elimu nchini.

Na hii si tu kwa shule za serikali bali shule zote hata zile zinazoitwa ni bora za binafsi, kinachotokea huko wanafunzi ni kuambulia kujua kiingereza tu.

Baadhi ya wasomi wengi bila kujali wasomea shule gani au chuo gani yaani wanekuwa ni mizigo ktk taifa hili.

Shida kubwa ktk elimu hapa Tanzania ni kutokuwa na mfumo bora na endelevu wa elimu nchini.

Leo hii ukiangalia shule zinazotangazwa kufanya vizuri ktk mtihani utashanhaa viongozi wamekuwa wakikimbilia kutengeneza cv zao za kuonekana wamefanya vizuri kwa shule za eneo lao la utawala ambapo ukizifukunyua utakuta ni matokeo feki ya kupikwa.

Kuanzia utawala wa awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa mwenyewe elimu ilianza kuchakachuliwa na kuwa yenye mitaala ya hovyo, kilichoangaliwa hapo ni wanafunzi wengi waonekane wanakwenda sekondari na si kwa kigezo cha ufaulu safi na kwa kiwango kinachotakiwa kimantiki ya elimu bora.

Hapa viongozi walikuwa kisiasa zaidi, walitafuta sifa kwa mataifa ya nje kuonekana tz tumepiga hatua, kumbe zilikuwa hatua za kurudi nyuma kwa kasi zaidi.

Elimu ya kujua kusoma na kuandika na si kuelewa mambo ya nduniani tunamoishi ni kwa namna gani vijana waweze kuitumia elimu yao kunufaika na ardhi tuliyopewa na mwenyezi mungu ni kuipoteza jamii ktk mwelekeo mzuri na kuipeleka gizani (kuzimu).

Wasomi wengi sasa hivi wamekimbilia siasa, siasa vijana wanahitimu masomo na kubaki mijini, muda wa uchaguzi unapofika ndipo wanakumbuka kwenda vijijini kwao.

Wasomi hawa wanakutana na changamoto ya kutokukubalika kutokana na kwamba muda mwingi hawashiriki shughuli za kijamii kwa jamii yao jambo ambalo wanajikuta wakionekana vituko na walaghai mbele za jamii zao.

Na kila wanaposhindwa wanakimbilia mijini tena kwenda kusubiri uchaguzi ujao, na ndivyo mambo yanakuwa magumu zaidi hata wanapothubutu tena.

Elimu isiyowaandaa vijana kujitegemea kwa kutumia fursa zinazowazunguka hiyo siyo elimu bali ni mchakato wa kuwapumbaza na kwaongezea ujinga zaidi vijana na kuwa mzigo mkubwa kwa taifa.

Maoni