Asasi Kiteto zatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu

Kamanda wa Uhamiaji Kiteto, Ikomba Mathew, akisisitiza kuwa raia ya kigeni wanaweza kupata ajira maalum nchini kisheria ambazo ni adimu huku watanzania wakitakiwa kujifunza katika nafasi hizo..
Joseph Mwaleba Afisa maendeleo ya Jamii Kiteto, amewataka wakuu wa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi kwa uadilifu




ASASI Kiteto zatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu

, MOHAMED HAMAD
MASHIRIKA yasiyo ya Kiserikali Wilayani Kiteto mkoani Manyara, yametakiwa kutafakari shughuli zao ili kuleta tija kwa wananchi katika kuwahudumia.

Akizungumza na viongozi wa mashirika hayo mjini Kibaya jana, Kamanda wa Uhamiaji Kiteto Ikomba Mathew alisema, masharika  yanatakiwa kuwa daraja kati ya Serikali na jamii.

“Mashirika yanafanya kazi kwa lengo la kuisaidia Serikali katika maeneo yalipo, hivyo yanapaswa kuendeleza jitihada hizo”alisema Kamanda Ikomba.

Aliwataka viongozi hao kutokuwa na ASASI za mifukoni, ambazo zitawanufaisha viongozi na badala yake ziwe kwa maslahi ya jamii sambamba na kulinda usalama wa wananchi, kwa kuajiri raia wazalendo wa Tanzania.

Endapo kutakuwa na hitaji la kuajiri raia wa kigeni, wameaswa kuzingatia nafasi ambazo watanzania watajifunza kutoka kwa wageni ili nao waje kuajiriwa .

Akizungumza katika kongamano hilo, Fadhili Magogwa, maratibu wa shirika la Elewa Afrika aliiomba Serikali kuendeleza miradi hasa ya maji ambayo inaonekana kudhorota mara inapokamilika na kukabidhiwa.

“Miradi mingi ya maji imedorora kwa kukosa usimamizi, wakati fedha nyingi zilizotumika kuigharamia, Serikali iwe na mkakati madhubuti kuhakikisha miradi hiyo haifi”ma hiyo”alisema Magogwa.

Mwadawa Ally Mratibu wa shirika lilisilo la kiserikali KIWOCOA, ambalo linafanya kazi ya kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake Kiteto, aliomba Serikali kutambua mchango wa mashirika bila kuwa na ubaguzi.

Mwisho.

Maoni