Baraza la biashara Kiteto laitaka Serikali kutenga maeneo ya viwanda

Na MOHANED HAMAD

Baraza la biashara Kiteto mkoani Manyara, limeishauri Serikali kutenga maeneo kwaajili ya uwekezaji wa viwanda.

Wakiwa katika kikao hicho mbele ya Ndaki Stephani,Katibu Tawala ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa baraza hilo walisema, hawajaona jitihada za Serikali kupata maeneo hayo.

Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine imeziagiza halm kutenga maeneo kwaajili ya uwekezaji wa viwanda hapa kwetu sioni jitihada hizo, alisema Kanti Gregory mjumbe

Alisema kila mara kumekuwepo na kauli tata juu ya utengwaji wa maeneo hayo kuwa kuna kiasi kilichotengwa lakini hakionyeshwi katika vikao hivyo

Kwa upande wake Ndaki Stephano, kaimu mwenyekiti wa kikao hicho, aliagiza halm kuwa makini katika mipango yao kwa lengo la kuhudumia umma.

Mbali na eneo hilo pia waliomba kutengewa eneo jipya la makaburi baada ya lililokuwepo kujaa

"Mhe mwenyekiti hapa mjini Kibaya, sioni jitihada za Serikali kupitia wataalamu wa idara ya ardhi kupatiwa eneo jipya la kuzikia

Kwa hali ya kawaida huwezi kuamini kuwa hapa nafasi zilizobaki za kuzikia ni tatu tu hawa wataalamu wala hawashtuki hili

Pia walimshauri wakala wa barabara vijijini Tarura Mhandisi Gerald Matindi, kuona namna ya kuanza ujenzi wa barabara kwani abiria wanapata adha kubwa katika safari zao.

Maoni