BAWACHA Manyara waungana na wenzao kusherehekea

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani baraza la wanawakela chadema mkoa wa Manyara tulifanyia maadhimisho hayo katika wilaya ya mbulu,

Shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuitembelea na kuifariji familia ya  aliyekuwa katibu wetu wa bawacha mkoa maremu Suzy

Tuliwapelekea nahitaji Kama sukari Mchele na Sabuni, na baadae kutembelea kaburi lake na kuweka shada, pili tuliweza kutembelea kituo cha Wagonjwa bashay kilichopo chini ya Padre James

Tulipanda miti katika maeneo hayo ya mabweni ya Wagonjwa, natulikutana na Wagonjwa na kuwafariji Kwa kuwapatia nahitaji Kama Mchele, Sabuni na soda,

Hakika walifarijika Sana na kikubwa padre pamoja na Wagonjwa walitusshukuru Sana sisi kufika kwetu huko na walituombea na kuliombea taifa letu Kwa ujumla,

Ujumbe wa padre kwetu alituomba tuliambie taifa kuwa siasa Si chuki Bali kutofautiana kwetu kiitikadi na kimtazamo isiingize taifa katika chuki na machafuko

Amesihi Sana tofauti zetu ziwe ni katika kuliletea taifa maendeleo badala yakukandamizana na kuumizana, ikumbukwe pia kauli mbiu yetu ya bawacha mkoa mwaka huu ni"

Wanawake tunahitaji haki na Amani katika taifa letu "  ....imeandaliwa na kaimu katibu bawacha mkoa wa Manyara, Sukarina martin.

Maoni