CCM Kiteto wafurahishwa na utekelezaji wa Ilani

CCM Kiteto waridhishwa na utendaji kazi wa halmashauri.

Na MOHAMED HAMAD 

CHAMA cha mapindinzi (CCM), wilayani Kiteto mkoani Manyara, kimeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaofanywa na halmashauri.

Jumla ya shilingi mil 180 zimeanza kutumika kujenga madarasa 16 na vyoo, shule ya Twanga, Kazingumu, ili kupunguza adha ya wanafunzi kusomea chini ya miti.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Kambona kati ya madarasa manne yanayojengwa, darasa moja linaongezeka kutokana mfumo anaotumika wa fosi akaunti.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Eng Pashue Shekue katibu  wa (CCM) Kiteto alisema, wananchi wanatamani kuona wakitunikiwa kikamilifu.

"Mkurugenzi Kambona, amekuwa mfano wa kuigwa hapa nchini, kwa kujiongeza kutumia fedha za wananchi vizuri katika ujenzi"

Kwa zaidi ya miaka sita, Kiteto tumekuwa tukitatuka migogoro ya ardhi zaidi kuliko kufanya shughuli za naendeleo.

Mkurugenzi Kambona umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuijenga Kiteto upya ambayo ilionekana viongozi wake kutowahudumia wananchi kutokana na migogoro ya ardhi.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi wakizungumzia naendeleo hayo waliahidi kushirikiana na Serikali kufikia malengo.

"Tuna zaidi ya miaka sita Kiteto tukilumbana kuhusu migogoro ya ardhi, huku naendeleo mengine yakisimama kutokana na hofu kwa watawala" alisema Rajabu Bakari (Mwananchi)

Mwisho.

Maoni