DC atishia kuhamisha fedha za ujenzi

DC Same ashawishika na ushauri wa wataalamu wa kutaka hela za kujenga bweni Shule ya sekondari ya Bombo zihamishiwe shule nyingine.

💤Hii ni kutokana na wananachi wa kata ya Bombo kutotoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha ujenzi wa bweni hilo unakamilika

💤Fedha za serikali ( P4R) zilipelekwa tangu mapema 2017 na mradi ulitakiwa kuisha Nov. 2017

💤DC alishiriki msaragambo wa kukamilisha kusawazisha eneo tangu Aug. 2017. Ikitegemewa kuwa kuanzia hapo ujenzi wa bweni uanze.

💤Alipotembelea shule hiyo  March, 2018 bado hata msingi haujakamilika kujengwa.

💤Watoa sababu zisizo na tija.
💤Wananchi hawajitokezi kwenye kusaidia kazi

💤 Mtendaji kama muhamasishaji hajitumi, awekwa chini ya ulinzi masaa 8.
Apewa siku 2 kuleta maelezo kwa nini asichukuliwe hatua.

Hela za Serikali zakaa bila kazi kwa muda mrefu. Zaichafulia jina Wilaya, Kwani tunaonekana wote ni wazembe.

💤 " Ni heri tushauri hela hizi zihamishiwe mahali ambako wananchi wako tayari kupokea maendeleo na kushiriki; kwani wanaohitaji fedha hizi ni wengi" Alisema DC Rosemary. 

💤 Viongozi wa kisiasa hawatoi ushirikiano, na wanachangia kufanya kazi ichelewe.

💤 " Serikali ya CCM ina dhamira njema na haina ubaguzi katika maendeleo. lakini wanaoletewa maendeleo wanaleta uzembe; nitamshauri Waziri hela hizi zipelekwe kumalizia shule ambazo wananchi wameshajitolea zinangoja umaliziaji" Asema DC huyo.

Shule hiyo ililetewa Tshs Milioni 245 kwa ajili ya kujenga madarasa 4, choo na mabweni 2. Ambapo tangu Aug. 2017  kazi ya ujenzi wa madarasa ilikuwa imekamilika. Lakini baada ya hapo hakuna kilichofanyika kwa miezi 7 sasa.

Huu sio utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano.

Maoni