DC Kiteto aonja adha za barabarani

NA MOHAMED HAMAD
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumain Magesa, ni mmoja wa walioonja adha ya barabarani baadabya gari lake kukwama

Akiwa katika moja ya eneo korofi ambalo limeanza kutengenezwa, kufuatia zaidi ya magari 30 kukwama mapema asubuhi hii mkuu huyo wa Wilaya amewaahidi wananchi hao kuwa Serikali italishuhulikia

Eneo hili liko kata ya Namelock wilayani Kiteto Mkoani Manyara, ambapo kila mwaka abiria hupata adha baada ya magari kukwama

Abiria hao wamemwomba mkuu huyo wa Wilaya kuona haja na namna ya kulishughulikia kikamilifu ili kuondokana na usumbufu wanaopata kila mara

Kwa mujibu wa Eng Matindi Gerald meneja Tarura Kiteto, alisema barabara hiyo iko katika mpango wa kutengenezwa na tanroad kwa kiwango cha lami, Narco KIteto Arusha hivyo wananchi wavute subra

Maoni