DC Kiteto awaasa wanawake..

Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Tumain Magesa, akiwashauri wanawake, ambao hawako pichani njia bora ya kuendesha familia zao kwa mashauriano na wenzi wao.
Mama Kalwani, makamu wa mwenyekiti wa kikundi cha ujasiriamali Kimanga, akisoma taarifa kwa mkuu wa wilaya, Tumain Magesa aliyewatembelea kuona shughuli zao

DC Kiteto awaasa wanawake


Na, MOHAMED HAMAD KITETO.

MKUU wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tumaini magesa, amewataka wanawake kuwa washauri wazuri wa waume zao kiuchumi ili kundokana na umaskini wa kipato katika familia.

Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo na wanaushawishi mkubwa kwa waume zao..ushawishi huo utumike vyema kuwashauri wapate maendeleo ili kuendeleza familia zao.

Akizungumza na kikundi cha ujasiriamali upendo katika mji wa Kibaya pamoja na wanawake wa Kijiji cha Mbigiri kata ya Partimbo DC Magesa alisema, uchumi katika baadhi ya familia umeshuka kutokana na wanaume kukosa ushauri mzuri.

“Wanawake mnanguvu kubwa ya ushawishi..mbona mkitaka kitu kwa waume zenu mnapata tena kwa wakati? kwanini msiwashawishi waondokane na kilimo kisicho na tija na ambacho ni cha mateso” alisema Magesa.

Baadhi ya wakulima, hulima ekari 100 na kupata mazao gunia 100 ama 50, jambo ambalo ni hasara kubwa, lakini utashangaa kila mwaka wanalima, kwanini wasilime ekari chache kitaalamu zitakazokuwa na tija?alihoji Magesa.

Mwajuma Bakari (mkulima) wa Kijiji cha mbigiri, aliambia MTANZANIA kuwa moja ya tatizo walilonalo wanawake ni kudharauliwa na badhi ya wanaume katika mipango ya uchumi.

“Ukimshauri mwanaume katika masuala ya uchumi hata kama ni jambo jema, anaweza kukuitikia na hatotekeleza kwa madai kuwa utamdharau mafanikio yatakapopatikana”alisema Mwajuma

Kwa upande wake Rehema Samweli, mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Kiteto, alimhakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa jukwaa hilo litatumika kuelimisha wanawake njia bora ya mashauriano katika familia zao.

Kilimo kinachofanyika Kiteto ni cha mahamba makubwa yasiyo na tija,  ambacho kinaibua migogoro kati ya wakulima na wafugaji, kwa kuona hilo Serikali wilayani Kiteto imeanza mkakati wa kuwataka wakulima kulima Kisasa

Mwisho.

Maoni