DC Mbulu ataka kuendelezwa uzalenzo

Mkuu wa wilaya ya mbulu chelestino s mofuga, marchi 17/2018 alikuwa mgeni  kuwaaga watumishi wa uthibiti ubora wa shule Anna Mahawe na Mwanaisha mnderi.

Watumishi hao walistaafu kwa mujibu wa sheria  na kuagwa rasmi na wenzao ili waweze kuendelea na majukumu ya kijamii.

Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza  watumishi hao ambao wasifu wao umeonyesha kuwa walikuwa waadilifu, wachapakazi, wazalendo na walifuata sheria, kanuni za utumishi kikamilifu.

Katika hatua hiyo DC Mofuga, aliwataka watumishi wa serikali walioshiriki hafla hiyo kutofanyakazi kwa mazoea ili kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari wetu wa mabadiliko Dkt John Pombe Magufuli ambaye anafanya kazi na kwa muda mfupi ameibadilisha Tanzania.

Pia amewaasa watumishi wastaafu kuwa wasisahau hata baada ya kustaafu kunahitaji uadilifu mkubwa, uchapakazi, uzalendo katika nchi.

Maoni