DED Kiteto ahidi neema
Na MOHAMED HAMAD MANYARA
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tamimu Kambona, ameahidi kutumikia wananchi kwa kiwango stahili.
Nimechimba visima 12 vya Maji, nimeanzisha Sekondari mbili za wanafunzi wa kidato cha tano na sita za Kiteto sekondari na Engusero, nimeboresha vituo viwili vya afya Matui na Sunya.
Huu ni mpango mkakati wangu kuihudumia jamii nikiwa kama mkurugenzi wa Kiteto kwa miaka miwili toka nimeteuliwa na Mhe Rais.
Alisena mfumo wa Serikali ya awamu ya tano ni mwepesi, kwani wanataka kuona matokeo ya kazi zaidi kwa wananchi ndipo watoe Pesa.
Nitapokea fedha nyingi mbali na kiasi cha mil 400 nilizopokea kuboresha kituo cha afya Sunya na zaidi ya mil 200 kuboresha sekondari ya Engusero, kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi hiyo.
Changamoto tuliyonayo ni kulazimika kutumia muda mwingi kutatua migogoro ya ardhi kuliko shughuli zingine za maendeleo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel (CCM), aliwahakikishia wananchi hao kuwa watanufaika na utawala uliopo kutokana na uwajibikaji wa viongozi hao.
"Kila kiongizi wa Serikali anahofu ya kutumbuliwa..wanalazimika kuonyesha elimu yao kuwatumikia wananchi zaidi tofauti na awali na sio vinginevyo" alisema Mollel.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni