Kiteto bado kuna madarasa ya chini ya miti

Wakati kukiwa na sera ya elimu bila malipo hapa nchini, baadhi ya maeneo hayapati huduma ya elimu kama inavyotakiwa.

Wilaya ya Kiteto, ilipanda kwa ufauli na kufikia asilimia 78% kutoka na sababu mbalimbali kiwango hicho kimeshuka hadi kufikia 58%.

Miongoni kwa sababu zilizotajwa ni pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa, nyumba za wakimu, uhaba wa walimu na vitabu.

Katika hatua hiyo baadhi ya shule ikiwemo ya Twanga kata ya Nameloko wilayani hapa yenye madarasa 3 imelazimika kuanzisha darasa jingine chini ya mti kunusuru hali hiyo

Kutokana na hali hiyo mkurugenzi mtendaji wa halm ya wilaya, Tamimu Kambona ameamua kujenga vyumba 3 vya madarasa kunusuru wanafunzi hao.

Maoni