LHRC waamsha dude la Katiba.

Fortunata Ntwele wa (LHRC) na Renata Selemani kulia wa kituo cha sheria na haki za binadanu (LHRC) katika majukumu yao ya kazi za kituo..

                  Warsha ya wasaidizi wa kisheria, katika kuihuisha mchakato wa katiba mpya



LHRC waamsha dude la Katiba.

Na.MOHAMED HAMAD.
KITUO cha sheria na haki za binadamu nchini (LHRC), kimeiomba Serikali kuhuisha mchakato wa katiba, ili kuthamini rasilimali fedha za wananchi zilizotumika, pamoja na kulinda mawazo ya wananchi yaliyotolewa.

Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 8 (1) (a) katiba ya 1977.

Kila raia ana haki na uhuru kushiriki kikamilifu kufikia maamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa, Ibara ya 21 (2), katiba ya 1977.

William Kahale wa Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC), akiwa na wasaidizi wa kisheria kutoka mikoani mjini Dodoma alisema, kutopatikana kwa katiba mpya kunaifisha mipango ya wananchi kutaka kuongozwa kikatiba.

Pamoja na jitihada kubwa zilizofanywa kutaka kuuhisha katiba hiyo toka kwa  wadau mbalimbali wakiwemo LHRC, walienda mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vya rasimu hiyo na kukubalika, ingawa bado mchangato huo hauonyeshi upatikanaji wake.

Bonny Matto msaidizi wa kisheria (Tarime) alisema, pamoja na rasimu hiyo kufikia hatua ya maamuzi ya wananchi kupigiwa kura na kuna mapungufu makubwa yakiwemo, Rais kuwa na madaraka makubwa pamoja na watu kutokuwa huru kutoa maoni yao.

Kwa upande wake, Pili Kuliwa (Kilwa) msaidizi wa kisheria aliwaasa wananchi kuonyesha hitaji la katiba hiyo kwa kusemea katiba katika maeneo yao ili Mhe, Rais aweze kumalizia mchakato huo ambao kwa sasa unaonekana kukwama.

Mwisho.



Maoni