Mnyeti aanza ziara Hanang, Manyara


Na MOHAMED HAMAD
Mkuu wa Mkoa wa Manyara mhe Alexander Pastory Mnyeti leo leo tar 12.3.2018 ameanza ziara ya siku tano Wilayani Hanang

Katika ziara hiyo atatembelea na kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero, ushauri na maoni yao.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara anazofanya mkoani humo, baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo

Katika ziara alizofanya Kiteto, SIMANJIRO, Mbulu na Babati, Mnyeti alisisitiza uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.

Kuhusu watumishi, mkuu huyo wa Mkoa aliwataka kuwatumikia wananchi ipasavyo kuondoa manunguniko.

Hayo yanaenda sambamba na kuchukuliwa hatua kwa watumishi wazembe ambao wanaonekana kutowajibika

"Mimi sio mkuu wa mkoa wa mabox, tuache siasa katika kazi..watumishi ninyi mmeajiriwa na wananchi, watumikieni lazima muwajali" kauli ya RC Mnyeti akiwa Kiteto wakati huo..

Maoni