Kamati ya Maafa yashuhudia uharibufu wa barabara na makazi Same.
Kamati yafanya ziara kuanzia Kijiji cha Makanya, Hedaru, Mabilioni Bendera, Kihurio, Ndungu, Maore, Kisiwani na Mkomazi kuona athari ya mvua zinaondelea kunyesha katika maeneo ya Wilaya hiyo.
Makanya Mvua yaziba daraja, yabomoa kingo za mto - Nyumba 115 zavamiwa na maji (Hakuna athari kwa binadamu ila mali)
Bendera, miundombinu ya barabara yaharibika, maji yakwepa daraja;
Maji yaingia ndani ya nyumba na kuharibu baadhi ya vifaa na mazao.
Nyumba zaanguka na kukosesha makazi Mgandu
Kihurio- Daraja lajaa maji na kusababisha magari kusubiri masaa.
Ndungu - Mkomazi- mvua kubwa zasababisha magari kukwama kwa masaa.
Majevu - makorongo yapanuka yahatarisha makazi, Chome njia haipitiki na maeneo ya milimani.
Watendaji wameagizwa kuleta taarifa mapema Wilayani mara maafa yanapotokea
Tanroad wahimizwa kuanza kushughilikia matatizo hayo.
Wananchi waelekezwa kuchukua tahadhari kunapokuwa na mvua kubwa kusubiri maji yapungue.
WEO/VEO wakumbushwa kuwaelimisha wananchi juu ya ujenzi wa nyumba imara kwani baadhi ya nyumba zilizoanguka hazikuwa imara.
"Hata hivyo yako mambo yatakayosubiri mpaka mvua zipungue na yako yanayoweza kutatuliwa sasa hivi, tunawaomba wananchi waelewe kuwa, tatizo hili si la mtu yoyote bali ni hali ya mazingira ambayo hakuna aliyejua;
Naambiwa kuwa mvua za mwaka huu ni kubwa sana kuliko miaka mingine na hali hii iko maeneo mengi ya nchi kama tunavyoona kwenye vyombo vya habari. Nawaomba wananchi tuwe wavumilivu na tuchukue tahadhari wakati serikali tunaendelea kuboresha miundombinu". Alisema DC wa Same.
Na hasa ukizingatia Rais wetu Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli amedhamiria kwa dhati kuondoa shida za watanzania, na anaendelea kuimarisha miundombinu kadiri nchi inavyopata uwezo. Tupeni nafani.
Ziara hiyo ilifanyika Jmosi Tar. 17/03/2018 ikijumuisha DC Same, Mratibu wa Maafa, Kamati ya Ulinzi, TARURA, TANROADS, M/ Jamii na Ujenzi.
Maoni
Chapisha Maoni