RC Mnyeti atoa siku 30 DC kutatua matatizo ya wananchi

MOHAMED HAMAD

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, amempa siku 30, Mkuu wa wilaya ya Hanang Bi. Sarah Msafiri, kutatua migogoro yote ya ardhi wilayani humo.

Akiwa Hanang kwenye ziara ya siku tano, Mnyeti alisema, migogoro yote ya ardhi itatuliwe ndani ya siku 30 ili kuonyesha Uwajibikaji wa viongozi.

"Niwachekeshe, nilipokuwa Arumeru, nilipigiwa simu..hongera sana mkuu wa wilaya unafanya kazi nzuti sana mpaka unatufunika..natamani ungekuja Manyara, sasa niko Manyara nakuagiza fanya kazi" alisema Mnyeti huku wananchi wakicheka

Kuhusu mashamba yanayomilikiwa na wawekezaji Mnyeti alitaka yaendelezwe mara moja la sivyo watanyang'anywa na kupewa wananchi

Suala la barabara nalo liliulizwa namna ya wakala TARURA, atakavyo zishughulikia na kuelewa kuwa wananchi wasiwe na hofu kuwa kazi itafanyika vyema.

Mwisho

Maoni