TAHOSA yapania kupandisha ufaulu Same

Kikao cha Wakuu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Same kimefanyika Tar. 21/03/2018.

Wamekusudia kutoka nafasi 21 hadi ya kumi bora kitaifa, kuongeza ufaulu toka nafasi ya 68 hadi 21.

Changamoto ya utoro wa wanafunzi imeeleza kama kikwazo cha ufaulu na kumuomba DC wa Same kuwa mlezi wao.

DC Same aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kikao hicho atoa zawadi kwa shule 3 za kwanza kwa ujumla na 3 za serikali

Awapongeza waliofanya vizuri kwa kuungana na kauli ya Same ya kutaka mabadiliko.

DC aeleza baadhi ya sababu zinazopelekea shule za binafsi kufanya vizuri kuliko za serikali

"Tulijaribu kufanya uchambuzi mwaka jana na tulijifunza kuwa watoto wanaokaa nyumbanj (day) wengi wana wanamaadili mabaya kuliko wale wa bording/ hostel kwani wazazi hawafuatilii ratiba za watoto kama Mwl.

Wanawaacha watoto waende wanakotaka bila kujali wanafanyanini na hii inapelekea  watoto kujiingiza kwenye mambo yasiyohusiana na masomo;

Wakati mtoto anayesoma bording muda wote ana ratiba inayojulikana na kufuatiliwa, hivyo kumpelekea mtoto kuzingatia masomo muda mwingi na kupelekea kufanya vizuri zaidi."

Na kwa kuwa shule nyingi za binafsi ni za bording ndiyo inawapelekea kufanya vizuri zaidi.

Alisema pia uzembe wa baadhi ya walimu ni changamoto na kutoa mfano wa matokeo ya 2016 ambapo baada ya hesabu somo lililofuata kwa matokeo mabaya ni history ambayo ina walimu hadi wa ziada, haina practical lakini bado wameshindwa kuwaelewesha watoto.

Alitoa wito kwa walimu wazembe kukaza buti kudhihirisha uwezo wao kwa vitendo. Maana siku zao zinahesabika.

Alikumbusha kumtendea haki Rais wetu Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali na watanzania kwani ameboresha Elimu pamoja na kuwapa posho ya madaraka.

Aliwataka WEO/ VEO kuwaelimisha wazazi juu ya chakula cha mchana ili wakae muda mwingi mchana wakiwa na uangalizi wa shule.

Aligawa kitabu cha maadili ya watoto wa kike kwa kila shule, na awaomba walimu kuendelea kuwaelimisha ili kuondokana na mimba

Alipongeza kwa takwimu zinazoashiria kupungua kwa mimba kulinganisha na 2017

Awataka shule zilizofanya vibaya kujithathmini ili kuongeza ufaulu na kuwakumbusha shule binafsi kubadilishana uzoefu na wenzao ili kufanya vizuri kama taifa.

" Huko nyuma matokeo yalipokuwa mabaya, kila mtu alimtaja mwenzake kuwa ndiye aliyefanya uzembe( walimu walisema ni serikali na wazazi; wazazi walisema ni walimu na serikali; na serikali tumesema ni wazazi na walimu wazembe

Lakini sasa tumefanya vizuri kila ninayekutana naye anaeleza jinsi alivyochangia /Alivyohusika na ufaulu huo, na kama ni hivyo basi kila mtu akubali pia alihusika kwa kufanya vibaya". Asema DC Same Mh. Rosemary Senyamule.

Aliwataka wadau wote kutimiza wajibu wao, ili tujivunie matokeo mazuri kwa pamoja kwamba Tanzania ya viwanda inahitaji wataalamu.

" Same is not same" ni hakika.

Maoni