Viongozi wa Dini Same wamuunga JPM

VIONGOZI WA DINI SAME WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS

Rais John Pombe Joseph Magufuli, ameungwa mkono na viongozi wa dini kusaidia familia duni.

Vijana hao wanafundishwa TEHAMA ya kiwango cha juu kwa ajili ya kujiajiri, kutengeneza robot zinazotembea - Robotics.

Wanatenganeza Aplikesheni za simu - App inventor, katuuni za kubuni wenyewe - Scratch Na Arduing.

Pia watengeneza App itakayotumika kueleza habari za Same na baadaye Tanzania.

Wanatengeneza maktaba ya kimtandao - e-library, ambapo walimu wanatoka Korea, Tanzania Na Marekani ambapo vijana waahidi kujiajiri.

Mratibu wa Shirika la Compassion ( Esther Mgimba) amesema shirika linafanya kazi na taasisi 4 za dini kwani wameona kujituma Na uaminifu zaidi kwao.

Na kuwa wameanzisha vituo 4 Wilayani Same vitakavyoendelea kutoa Huduma za e-library.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka watumishi wa halmashauri kuanzisha maktaba kama hiyo  Wilayani kutokana na kutokuwa nayo.

Amewataka vijana waliohitimu kuendelea kufanyia kazi waliyojifunza kwa maendeleo ya viwanda.

🔵Aliwasisitiza watengeneze jembe la robot kutokana na vijana wa sasa kutoshiriki shughuli za kilimo, kwa kila Program ianzishe kiwanda

Mchungaji Munisy wa kanisa la TAG apongeza ushirikiano uliopo kati ya serikali na Taasisi hizo za dini.

Shughuli hiyo ilifanyika Tar. 29/03/2018 Katika darasa la TEHAMA lililopo kanisa la TAG.

Maoni