Wanawake Same waungana na wezao siku ya wanawake

Wanawake Wilaya ya Same waungana na wanawake wote kusherehekea siku ya wanawake Duniani.

💃🏼Makundi ya wanaweke kuanzia shule ya msingi, sekondari, vyuo, wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wanasiasa, viongozi katika nyanja zote;

Wanakubaliana kuhakikisha Wilaya ya Same inawaandaa wanawake kushika  nafasi nyingi zaidi za juu katika uongozi na kuwa kati ya wanawake wanaomiliki biashara kubwa nchini.

Wasema kumiliki viwanda ni haki yao.
Wahamasisha kuanza kutafuta maeneo ya uwekezaji

💃🏼Kufikiria kukua zaidi, kuchukua hatua bila kusubiri, kushikana mkono.
💃🏼Serikali ya Wilaya yajipanga kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali kuu.

💃🏼Yaanza kuunda mabaraza ya kata, yaanza kutenga maeneo ya uwekezaji vijijini na kuainisha maeneo ya wanawake, yaahidi kutoa % ya wanawake,  vijana na walemavu kwa ukamilifu.

💃🏼 Yapanga kuanzisha soko la barabarani kukuza bidhaa za wanawake.

💃🏼Yashirikisha wadau kujenga majengo ya kuwezesha viwanda vya wanawaje.

💃🏼Yahidi kutetea haki ya elimu kwa watoto wa kike.

💃🏼 Mkuu wa Wilaya ya Same Mh. Rosemary Senyamule, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo apongeza ushirikiano wa wadau juu ya kumtetea mtoto wa kike, uliofanikisha kifungo cha miaka 30 kwa watuhumiwa 2 mwezi Feb. 2018( 1 kwa kosa la kuoa mwanafunzi na mwingine kwa kosa la kubaka).
Pia asema mimba kwa wanafunzi zinaonyesha dalili ya kupungua 2018.

💃🏼Asema sasa tuwatie nguvuni wanaowapa mimba wanafunzi ili nao wapate fundisho.

💃🏼Aahidi vyombo vya ulinzi kuendelea kuwasaka wote.

💃🏼 Awataka wanawake Same kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Wilaya kwani wengi ni wanawake, wakiweza ni ushindi kwa wanawake wote.

💃🏼Ampongeza  Rais kwa heshima aliyowapa wanawake katika nafasi za uongozi na kuwaomba wanawake wote kufanya vizuri ili wengine wapewe pia.

Baada ya sherehe ya mchana, Sherehe ya kujipongeza kuzaliwa mwanamke yaendelea hadi jioni

" Leo nimewaombea wanawake wote ruhusa kuja ili mjifunze wanawake wenzenu wanafanya nini" Wanaume leo waacheni wanawake wafurahi" Ni maneno ya Mh. Rosemary.

"Same is not same"

Maoni