Watumishi Kiteto watahadharishwa..

Tamim Mahmoud Kambona, Mkurugenzi wa Kiteto akiwasihi watumishi wa Serikali ya wilayani humo kufanya kazi kwa uadilifi ili kuendana na kasi ya Rais Dr. John Pombe Magufuli..


Madiwani wa halm ya Kiteto wakifuatilia kikao, ambapo pamoja na mambo mengine walitakiwa kila mmoja awajibike katika nafasi yake..





DED Kiteto sikotayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa mwenzangu.
Na, MOHAMED HAMAD

MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tamim Mahmoud Kambona, amewatahadharisha watumishi wa Serikali wilayani humo kuwa, hatokuwa tayari kusimamishwa kazi kwa uzembe wa mtu mwingine.

Mkurugenzi Kambona ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mjini Kibaya kuwa, Serikali ya awamu ya tano inataka kila mtumishi awajibike katika eneo lake.

“Haitokuwa vizuri sana inapoonekana kusimamishana kazi, kwani inamfanya mtu kukosa fursa na imani ya kuaminika katika maeneo mengine, kwani muundo wa Serikali yetu mnauona jinsi hatua zinavyochukuliwa kwa wasiowajibika” alisema Kambona.

Alisema wakati mwingine aliyechini anapokosa kutumiza majukumu yake anayechukuliwa hatua ni  mtu wa juu kwahiyo..., mimi mwenyekiti sipo tayari linikute la aina hii.

“Naona wazi kuwa mwakani, kama tutapata hati chafu ni kwasababu ya chapa ya mifugo, niwatake wakaguzi mfanye kazi kwa umakini, atakapokuja mkaguzi, atataka kujua  kuhusiana na chapa ya mifugo sipendi  uonevu kwa yoyote”

Alisema aliyehusika na zoezi hilo hata kama hajasimamishwa kazi, akaonekana kula fedha hatosita kumchukulia hatua..akisema alikuja peke yake na atarudi peke yake, sipendi kuona mtumishi anaonewa au ananyanyasika au amekosa stahili zake, alisisitiza.

Watumishi wa Serikali wasitoe nafasi kwa madiwani kuwalalamika kwa mambo ambayo yanatakiwa wayatekeleze..hakuna sababu ya kusukumwa kufanya kazi hiyo wakati ni wajibu wao, huku akiongea kwa hisia.

Pia aliwataka wana Kiteto kusomesha watoto wao ili waweze kufanya kazi katika mazingira yao, kwani zinapotoka nafasi za ajira na kukosekana mtu mwenye sifa inatoa nafasi kwa vijana wa maeneo mengine kupana nafasi hizo


Maoni