Waziri Nyongo aifungia kampuni ya madini Kagera




Naibu Waziri Nyongo aifungia kampuni ya madini Kagera.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, amemwagiza mmiliki wa kampuni inayochakata madini bati ya (African Top Minerals), iliyopo Kyerwa mkoani Kagera, Hassan Ibar, kutoendelea na kazi hiyo hadi atakapofuata taratibu za kuomba na kupatiwa leseni halali ya Serikali. 

Agizo hilo lilitolewa jana, feb 28, alipotembelea na kukagua kampuni hiyo na kubaini kapuni hiyo kutokuwa na leseni akiwa katika ziara yake ya kazi mkoani Kagera. 

Naibu Waziri alimwambia mmiliki huyo kuwa, Serikali inapenda wawekezaji wawepo ili pamoja na mambo mengine wasaidie upatikanaji wa ajira kwa wananchi lakini akaonya kuwa haiwezi kuridhia mtu yeyote kufanya uwekezaji pasipo kuwa na leseni halali itakayomwezesha kutambuliwa na Serikali na kulipa kodi zote stahiki.

Mwisho..


Maoni