FAHAMU MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI ZA SERIKALI KITETO

Mradi wa ujenzi ofisi za Serikali wilayani Kiteto mkoani Manyara, unetajiwa kuwa wa kihistoria

Gharama halisi za ujenzi huo zimetajwa kuwa ni bil 4.3, kwamba utaratibu unaotumika ni wa fosi akaunti

Kwa mujibu wakuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumaini Magesa, alisema ameridhishwa na kazi ya ujenzi na kuwataka jitihada hizo ziendelee

Amesema kila mara amekuwa akifanya ukaguzi na kushauri, panapohitajika na kuongeza Serikali imeridhishwa na kazi ya ujenzi inazofanywa na Mkurugenzi wa Kiteto

Akizungumza mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya, Tamim Kambona Mkurugenzi wa halm ya Kiteto aliomba Serikali kutoa Fedha kwa wakati mara inapofikiwa hatua ya malipo ili ujenzi uendelee

" Mhe Mkuu wa Wilaya changamoto iliyopo hapa ni kuchelewa kupata Fedha toka Serikalini, hali hii inafanya ujenzi kusuasua..naomba Serikali ilitusaidie kupata Fedha hizi kwa wakati"

Baadhi ya wananchi wilayani Kiteto wamepongeza jitihada za Serikali kujenga jengo la kisasa wakisema hayo ni maendeleo

Katika hatua hiyo wamemshukuru Tumain Kambona Mkurugenzi mtendaji wa halm ya Kiteto kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo

Mwisho.

Maoni