HATUTAKI KUPOTEZA TEMBO TENA KWA UJANGILI.

HATUTAKI KUPOTEZA TEMBO TENA KWA UJANGILI.

Ni kikao cha ujirani mwema kati ya nchi ya Tanzania na Kenya kilichoshirikisha serikali, taasisi za serikali, NGOs na wataalamu na wadau wa wanyamapori.

Katika kikao hicho wajadili namna bora ya kuendelea kumaliza tatizo la uwindaji haramu kwa nchi zote mbili.

Wapongeza juhudi zinazoendelea serikalini zilizopelekea kupungua kwa ujangili.

Imeelezwa kuwa maazimio yatatolewa ya kutekeleza kwa pamoja, kwa wananchi wanaozunguka maenei

" Ni lazima tutoe uzito stahili kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya wanyamapori; wajue umuhimu wa wanyama hao.

Tuwape njia mbadala za kipato; Tuwahakikishie usalama wao wanapotoa taarifa za ujangili.

Wakielewa hawa watafanya kazi yetu iwe rahisi kwani watatupa taarifa nyingi za wahalifu na tutaweza kuchukua hatua mapema" . 

Hayo yalisemwa na DC Same, aliyekuwa mgeni rasmi kufungua  kikao hicho. 

Kuendelea kuwepo kwa soko la nyara hizo kwatajwa kama moja ya kichocheo cha kuendelea kwa ujangili. Pia bei kubwa sokoni.

Kikao hicho kimefanyika Tar. 11/04/2018 Wilayani Same.

Maoni