Serikali imeboresha kituo cha Afya Sunya, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, kwa kuongeza majengo matano.
Lengo la kuongeza majengo hayo ni kupunguza adha na usumbufu kwa wananchi ya kupata huduma ya Afya mbali
Zaidi ya mil 400 zinatumika kuboeresha kituo hicho, kujenga majengo hayo kwa wakati mmoja, kuwaondolea adha wananchi hao
Awali wananchi hawa wanalazimika kwenda Wilaya ya kilindi mkoani Tanga kusaka huduma ya upasuaji na kuongezewa Damu hali iliyo wapa usumbufu mkubwa
Akizungumza mbele ya mkuu wa Wilaya Omari Puputo (mwananchi) kuwa kituo hicho kikikamilika kitawasaidia wananchi na wataindika na adha kubwa
Kwa mujibu wa uongozi wa wikaya zaidi ya wananchi elfu 30 kutoka nje na ndani ya kata ya Sunya watapata huduma ya afya
Akizungumza na wananchi hao, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa, aliwataka watambue kuwa wamepata kituo bora ambacho hakuna mfano hapa nchini
Aliwataka wananchi hao kuwa na uchungu na kituo hicho kabla ya MTU mwingine hajajitokeza kuwasaidia
Kwa upande wake Dr Mwanaidi, wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto alieleza kuwa kituo hicho kina vyumba maalumu vya kujifingulia, ambavyo hakuna mfano wake hapa nchini
"Hapa kuna vyumba maalum vya kujifulia akinamama, ambavyo huwezi pata kokote nchini, hivyo nawataka wananchi kujivunia kituo hiki na kukilinda"
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni